Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juma Abdul achimba mkwara

Muktasari:

  • Yanga itacheza na Gor katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na Abdul amesema pamoja na kuchelewa kujiunga na kikosi hicho kutokana na changamoto ya mkataba, lakini alikuwa akifanya mazoezi ya peke yake ili kujiweka sawa.

BEKI wa Yanga, Juma Abdul, amejiunga na kikosi chake baada ya kumalizana na mabosi wake huku akichimba mkwara mzito kwa Gor Mahia ya Kenya kwamba wajiandae tu kisaikolojia katika pambano lao litakalopigwa Jumatano ijayo huko Kenya.

Yanga itacheza na Gor katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na Abdul amesema pamoja na kuchelewa kujiunga na kikosi hicho kutokana na changamoto ya mkataba, lakini alikuwa akifanya mazoezi ya peke yake ili kujiweka sawa.

Alisema anaamini kuelekea kwenye mchezo huo mgumu wa Kundi D hawatafanya makosa kwani kikosi chao hakina mabadiliko makubwa kutokana na usajili wao walioufanya.

“Mkataba wangu ulimalizika na sasa nimemalizana na viongozi wangu juu ya mkataba mpya, nimerudi na nitatumia muda huu mchache uliobaki kuongeza uzoefu na kujifunza mbinu mpya ya mwalimu kwa lengo la kuhakikisha nafanya vizuri zaidi,” alisema beki huyo.

“Kitu kikubwa ninachoweza kusema ni kuwatoa wasiwasi mashabiki wetu, Yanga ni timu kubwa kwahiyo hata kama imefanya vibaya katika ligi tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, kikubwa kwa sasa ni kujipanga kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri tushirikiane kwa pamoja kuleta ushindi. Hii ni timu ya ushindi.”

Kwenye michuano hiyo ya kimataifa, Yanga inaburuza mkia katika kundi lake ikiwa nyuma ya vinara USM Alger ya Algeria, Gor Mahia na Rayon Sports ya Rwanda.