Kocha Msaidizi Mwadui FC afariki dunia
Muktasari:
Ntambi ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Biashara Shinyanga, amefariki katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
Uongozi wa Mwadui umethibitisha kifo cha Kocha Msaidizi wa Mwadui FC,
Jumanne Ntambi ambaye amefariki dunia mjini Shinyanga.
Ntambi ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Biashara Shinyanga, amefariki katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
Taarifa zinasema aliugua muda mfupi na alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo ambalo liligundulika mwishoni.
Ntambi enzi za uhai wake alikuwa mwajiriwa wa klabu ya Mwadui FC. Endelea kufuatilia ukurasa huu kupata taarifa zaidi.