Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamkomalia kiungo wa Stand United

Muktasari:

  • Huku Stand United kiungo huyo anatambulika kwa jina la Afidh Mussa akisajiliwa kwa leseni namba 000238M93 ambayo ameitumia mpaka katika mchezo dhidi ya Yanga uliopigwa katika Uwanja wa Kambarage Shinyanga na vinara hao kulala 1-0 kwa Chama la Wana.

VINARA wa Ligi Kuu, Yanga jioni ya leo Alhamisi itashuka Uwanja wa Taifa, kuvaana na Biashara United katika mechi ya Kombe la FA, lakini kama ulikua unadhani mabosi wa klabu hiyo wameipotezea ile ishu ya kiungo wa Stand United, Afizi Mussa utachekwa.

Unaambiwa mabosi wa klabu hiyo wameikomalia ishu hiyo na juzi kati wamenasa ushahidi unaothibitisha kiungo huyo ni Mrundi, licha ya kwamba alizaliwa Tanzania baada ya leseni yake aliyokuwa akiitumia wakati akicheza Ligi Kuu ya Burundi kuonyesha mpaka jina lake la Kirundi.

Wakati Yanga ikinasa usahidi huo ambao Mwanaspoti imefanikiwa kupata nakala yake, Idara ya Uhamiaji haikulaza damu kwa kudaiwa kumnasa na kumhoji kwa muda kiungo huyo kabla ya kumuachilia, huku ikielezwa amepigwa pini asitoke nje ya Mkoa wa Shinyanga.

Ipo hivi. Taarifa kutoka Shinyanga ni kwamba, Afidh alishaitwa Idara ya Uhamiaji mkoani humo kwa mahojiano ya haraka kisha kuachiwa kwa dhamana kwa sharti la kutotakiwa kutoka nje ya mji huo.

Lakini wakati mambo yakiendelea hivyo huko Shinyanga, huku jijini Dar es Salaam Yanga wakavinasa vielelezo vingine vya Afidh kuthibitisha kuwa sio raia wa Tanzania kwa sasa.

Vielelezo hivyo ambavyo Mwanaspoti limevinasa pia ni leseni ya mchezaji huyo kutoka Shirikisho la Soka Burundi ikionyesha mshambuliaji huyo alicheza Ligi Kuu nchini humo akitambulika kama raia wa Burundi na ni mwaka juzi tu, yaani 2017.

Leseni hiyo inaonyesha Afidh akitambulikia kwa jina la Harerimana Afizi Mussa akiwa na uraia wa Burundi akitokea eneo la Cibitoke leseni hiyo ikitolewa tarehe 14/09/2017.

Huku Stand United kiungo huyo anatambulika kwa jina la Afidh Mussa akisajiliwa kwa leseni namba 000238M93 ambayo ameitumia mpaka katika mchezo dhidi ya Yanga uliopigwa katika Uwanja wa Kambarage Shinyanga na vinara hao kulala 1-0 kwa Chama la Wana.

Kupatikana kwa vielelezo hivyo vinaweza kumweka matatani zaidi kutokana na utofauti wa majina yake yote yanayopatikana katika leseni zake hizo mbili.

Mara baada ya Mwanaspoti kunasa nakala hiyo ya leseni na taarifa za kuhojiwa Uhamiaji, lilimsaka kiungo huyo lakini aligoma kuzungumza inshu hiyo na alipobanwa zaidi aliamua kukata simu.

“Siwezi kuzungumza lolote kwa sasa, niacheni jamani,” alisema Afidh na kukata simu, lakini Mwenyekiti wa Stand, Dk. Ellyson Maeja ambaye alikiri mchezaji huyo kuhojiwa, lakini hana taarifa zozote za kuzuiwa kutoka nje ya Shinyanga.

“Ni kweli aliitwa kuhojiwa, lakini tayari ameshaachiwa na tunaye kambini tukijiandaa na mchezo wetu wa Ligi Kuu Bara unaochezwa kesho (leo) Alhamisi, hizo taarifa za kuzuia kutoka Shinyanga kama klabu hatuna,” alisema Dk Maeja.

Yanga iliamua kumkatia rufani mchezaji huyo baada ya kunasa taarifa za siri kwamba hakuwa Mtanzania kufuatia kuubadilisha uraia wake alipoenda kucheza soka Burundi na kwamba hata, Amissi Tambwe anayetokea nchini humo alinukuliwa kucheza naye timu ya taifa ya nchi hiyo.

Hata hivyo viongozi wa Stand United walinukuliwa wakiibeza Yanga kwamba inapatapata kwa sababu ya kipondo walichowapa Kambarage, lakini ukweli ni kwamba Afidh ni Mtanzania aliyezaliwa Temeke na wanashangaa wapinzani wao kumng’ang’ani.