Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salamba kufanyiwa vipimo zaidi

Muktasari:

  • Salamba alishindwa kuendelea na mchezo jana baada ya kuumia goti la mguu wake wa kulia na nafasi yake kuchukuliwa na Medie Kagere.

Shinyanga. Mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya kitabibu zaidi kuhakikisha afya yake inakaa sawa.

 Salamba aliumia jana Jumapili wakati timu yake ikicheza dhidi ya Stand United walioshinda mabao 2-0, ambapo alishindwa kuelendelea na nafasi yake kuchukuliwa na Medie Kagere.

Chipukizi huyo alishindwa kuendelea ikiwa dakika 45 ambapo baadaye timu zikiwa mapumziko alichukuliwa na gari la wagonjwa 'Ambulance' na kupelekwa hospitali.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa licha ya kwamba afya ya mchezaji huyo kuwa nzuri kwa sasa lakini huenda akafanyiwa vipimo vya kina ili kumuweka sawa.

Ameongeza kuwa taarifa za awali za kitabibu hazikubainisha tatizo lolote kubwa,hivyo baada ya kuwasili leo Dar es Salaam wataangalia namna ya kufanya.

"Jana hiyo hiyo alipelekwa hospitali na kurejeshwa kambini baada ya vipimo kutobaini tatizo kubwa lolote kwa sababu alipata majeraha kidogo kwenye goti la kulia, ila kwakuwa tumefika Dar es Salaam lazima afanyiwe vipimo zaidi kwahiyo tunasubiri kuona kama itakuwa hapa Tanzania au nje ya nchi" amesema Rweymamu.