Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hiki ndicho kilichomkwamisha Mkandala kutua Yanga

Muktasari:

Yanga ilikuwa inahitaji huduma ya kiungo wa Prisons, Cleoface Mkandala lakini wakajikuta wanagonga mwamba baada ya viongozi wake kumkatalia.

Dar es Salaam.Kiungo wa Prisons, Cleoface Mkandala amefichua kilichomkwamisha asitue Yanga licha ya kufanya mazungumzo na mwenyekiti Dk Mshindo Msollo.

Mkandala anamaliza mkataba wake Prisons msimu huu, amesema haikuwa rahisi kwa viongozi wake kumwachia kutokana na kuhitaji huduma yake.

Amekiri walifanya mazungumzo na Dk Msolla, lakini yeye hakuwa na nguvu kwa kuwa alikuwa mali ya Prisons, hivyo aliacha viongozi wamalizane.

"Kama bado wataendelea kunihitaji basi watanichukua nikiwa huru kwa sasa nisingeweza kufanya lolote kwa sababu nina mkataba nao."

Amesema anaamini atafika mbali kwa sababu soka ni kazi yake, hivyo popote anapohitajika atafanya kazi.