Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msipojipanga Makambo atawalaza mapema kabisa

Muktasari:

Ingawa mashabiki wa timu ya Simba wanamhofia zaidi Mshambulia Amisi Tambwe kuelekea kwenye mchezo wa jumapili, lakini Heritier Makambo anaweza akawa mwiba mkali kuliko mshambuliaji yoyote kwenye mchezo huo.

INGAWA mashabiki na hata viongozi wa Simba wanamchukulia poa Heritier Makambo kwa vile hofu yao kubwa ipo kwa Amissi Tambwe aliyerejea upya, lakini Mkongo huyo amezisikia kejeli na amejipanga kumaliza kazi mapema.

Makambo anafahamu yeye na Meddie Kagere wa Simba ndio watakaokuwa wakitupiwa macho katika mechi ya watani hapo Jumapili, lakini amesisitiza anataka heshima kwa mashabiki wa Yanga na lazima aimalize Simba Uwanja wa Taifa.

Kuelekea mchezo huo wa 101 kwa klabu hiyo tangu zianze kukutana katika Ligi 1965, Makambo alisema katika kitu ambacho atafurahi zaidi ni kuona anapata nafasi na kuifunga Simba kwani litakuwa jambo kubwa zaidi kwake.

Makambo alisema anajua amesajiliwa Yanga na nafasi yake anayocheza ni ya kufunga kwa kila mechi, hivyo hatafanya makosa Jumapili ili kuisaidia timu yake.

Alisema anafahamu Simba ni timu nzuri yenye mabeki wazuri wa kati kama Pascal Wawa na Erasto Nyoni, lakini amejianda kushindana kuipigania Yanga.

“Kambi tuliyopiga hapa Morogoro ni kwaajili ya kupata muda mzuri wa kutuliza akili na kuusubilia kwa umakini mchezo huo, hivyo naamini nitafanya vizuri Jumapili,” alisema Makambo mwenye mabao mawili mpaka sasa.

Makambo alikosa mchezo uliopita wa Yanga na Singida United kutokana na majeruhi, hivyo Amissi Tambwe kupata nafasi ambayo Mrundi huyo aliitumia vyema vyema kwa kufunga mabao mawili, yaliyowapagawaisha Simba.

Simba wanaujua mziki wa Tambwe, ambaye msimu uliopita hakung’ara kwa vile alikuwa majeruhi, lakini kurudi kwake upya na kutupia mabao mawili yamewapa presha mashabiki wa Msimbazi kuelekea siku hiyo.