Kagere freshi, Makambo achomolewa Yanga

Saturday May 11 2019

 

By SADDAM SADICK

MWANZA. STRAIKA wa Mwadui FC,Salim Aiyee amewataja nyota wa Simba, Meddie Kagere, Emanuel Okwi na John Bocco mmoja wapo kubeba tuzo ya mfungaji bora, huku akimchomoa Heritier Makambo wa Yanga kwenye vita hiyo msimu huu.

Aiyee ambaye alianza kwa kasi msimu huu na kuongoza kwa muda mrefu kwenye orodha ya ufungaji mabao kwa kupachika 16, kwa sasa ameshaachwa nyuma mabao manne na Straika wa Simba Meddie Kagere.

Kabla mechi za jana Ijumaa Kagere alikuwa na mabao 20, Makambo (Yanga) akiwa na 16 sawa na Aiyee (Mwadui) na Bocco akiwa na 14 sawa na Okwi wote wa Simba. Akizungumza na Mwanaspoti, Straika huyo alisema kwa hali ilivyo ni wazi nyota wa Simba, Kagere, Okwi na Bocco mmojawapo anaweza kubeba tuzo hiyo lakini kwa Makambo wa Yanga hawezi kufurukuta.

Alisema sababu ya kuwapa nafasi wachezaji wa Simba ni kutokana na kuwa na mechi nyingi lakini hata kombinesheni yao inatisha sana lakini pia wana uwezo hata kiuchumi.

“Sijakata tamaa, lakini kiukweli Kagere, Okwi na Bocco mmoja wapo anaweza kubeba tuzo ya mfungaji bora, Makambo hapana hayumo kabisa, wale Simba kombinesheni yao ni nzuriîalisema Aiyee.

Pia mshambuliaji huyo alieleza kuwa kupungua kwa kasi yake kwenye ufungaji mabao ni kutokana na mechi nyingi za ugenini kuwa na changamoto nyingi ikiwamo kukamiwa, alikiri ushindani msimu huu umekuwa mkali kutokana na ongezeko la timu.

Advertisement

Advertisement