Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO>>>EXCLUSIVE: Zahera ampiga 'stop' Chirwa Yanga

Muktasari:

Kocha mkuu amesema ingawa hataki Chirwa arudi Yanga lakini bado atasajili mshambuliaji mpya atakayeweza kuisaidia timu hiyo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema  suala la kusajiliwa kwa mshambuliaji raia wa Zambia Obrey Chirwa limefungwa rasmi.
Zahera amesema leo katika kambi ta timu hiyo kwamba hataweza kumchukua Chirwa kufuatia Nidhamu ndogo ya mshambuliaji wake huyo wa zamani.


Zahera amesema amefanya uchunguzi kutoka nchini Misri ambako Chirwa alikwenda kucheza soka na kubaini ameamua kuondoka huko baada ya klabu yake imeshindwa kumlipa.


Zahera amesema kitendo cha Chirwa kurudi Yanga ni kama anarudi sehemu ambayo aliikimbia awali na kuleta usumbufu uleule.
Amesema ingawa hataki Chirwa arudi Yanga lakini bado atasajili mshambuliaji mpya atakayeweza kuisadia timu hiyo.

Aidha Zahera amesema uwepo wa mshambuliaji huyo hapa nchini amejulishwa kwamba amevunja mkataba na klabu yake baada ya kushindwa kukubaliana katika malipo yake baada ya kuingia mkataba.