Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco, Kagere utasoma ramani

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amerejea kuangalia mchezo wao wa mjini Kitwe, Zambia na kubaini kuwa kuna mambo hayakwenda sawa na ghafla akatoa maagizo kwa mastraika wake kabla ya kurejea nchini kurudiana na Nkana FC.

Kocha huyo amebaini kuwa hawakustahili kupoteza mchezo wao wa ugenini kwa mabao 2-1, lakini anaamini kama Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi watatulia kwenye mechi yao ya Jumapili, Nkana atapasuka mabao mengi tu.

Mbelgiji huyo ameamua kuwa kazi maalum nyota wake hao na wengine wa Simba ili kuhakikisha wanapindua meza na hapo ndio unaweza kuamini kabisa Jumapili kuna mtu atapasuka Uwanja wa Taifa.

Aussems alisema dakika 90 kwake ni kama kipindi cha kwanza cha vita yao na Nkana na kwamba wanasubiri kumaliza ngwe ya pili nyumbani na ametaka mastraika wake kushambulia mwanzo mwisho ili kupindua matokeo.

“Timu yangu ina wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kushambulia ndio maana hata kwenye mechi ya ugenini tulifanya hivyo, japo tulipoteza nafasi nyingi, hivyo nataka mchezo wa nyumbani tushambulie zaidi ili kupata mabao ya kutuvusha,” alisema.

Alisema kina Kagere wamekuwa wakifanya vizuri na kuelekea mchezo huo wa marudiano anaamini atatumia mazoezi yao kuweka mambo sawa ili kuhakikisha wanashinda nyumbani na kutinga makundi ambayo ndio kiu yao kubwa kwa sasa.

Nyota hao wa Simba waliorejea alfajiri ya jana kutoka Zambia wamekuwa wakifanya vizuri ambapo Bocco amefunga mabao matatu kama kiungo Cletous Chama, huku Kagere akitupia mawili na Okwi moja.

MSIKIE BOCCO

Nahodha wa Simba, John Bocco alisema nafasi ya kufuzu ipo tena kwa upande wao wamerudi kucheza nyumbani na kama wachezaji watapambana zaidi ya mechi ya kwanza ili kupata kile ambacho wanahitaji.

“Kama wao waliweza kupata matokeo ya ushindi wakiwa kwao naimani kubwa na timu yetu pamoja na benchi la ufundi kuwa tunaweza kupata matokeo mazuri zaidi kwetu,” alisema Bocco ambaye ndiye aliyefunga bao katika mechi ya ugenini.

Msimu uliopita Simba waliondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry katika hatua ya pili kwa sheria ya bao la ugenini.

MBELGIJI APEWA MBINU

Katika mchezo wa Kitwe, Simba ilitumia mfumo wa 4-3-3 dhidi ya Nkana, kitu kilichomficha kabisa kiungo wao, Chama mbele ya viungo wa wapinzani wao na sasa Kennedy Mwaisabula alisema Simba wana mlima mkubwa wa kupanda ili kuingia makundi, lakini kazi itakuwa rahisi kwao kama Aussems atabadili mfumo wake ikiwa ni pamoja na kumpumzisha Paschal Wawa na kumtumia Juuko Murshid beki ya kati.

Mwaisabula alisema hata viungo anapaswa nyumbani kutumia viungo watano tofauti na alivyowatumia watatu Chama, James Kotei na Jonas Mkude.

“Chama asingeweza kufanya vizuri mechi hiyo maana alikuwa anacheza na watu wanaomfahamu vizuri, mbaya zaidi kocha aliweka viungo wachache ndiyo maana walibanwa sana katikati kuliko wenzao waliokuwa wanafunguka zaidi.

“Kingine Simba hawapaswi kukaa na matumaini ya kubebwa na faida ya goli la ugenini, huko ni kujipoteza na kujiondoa kwenye mstari, bali wanatakiwa kufanya maandalizi kwa kuweka mawazo kuwa walipoteza mechi ya kwanza,” alisema.

Naye Dk Mshindo Msolla alisema, “Ni kweli wamepata faida ya bao la ugenini lakini Nkana ni timu inayonekana kuwa na uwezo wa kushinda hata ugenini, waliifunga UD Songo kwao Msumbiji. Muhimu pia ni namna ambavyo kocha atafanyia kazi kasoro za mchezo wa jana (juzi). Anatakiwa ashambulie zaidi kwenye mechi ya nyumbani.

“Kwa mfano Chama alishindwa kufurukuta kama matarajio ya wengi kwasababu alikutana na wachezaji wanaomfahamu kuliko hata wenzake wa Simba, ilikuwa ni lazima mechi hiyo apate tabu sana, ila wana nafasi ya kusonga mbele endapo tu watajitambua na kocha atafanyia kazi mapungufu,” alisema Dk Msolla.