Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amunike amesikia kilio chenu

Muktasari:

Baada ya muda mrefu watanzania kuwa watazamaji wa Mashindano mbalimbali, kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike ataka kuwa washiriki.

Licha ya kwamba mshambuliaji Eliud Ambokile ameonyesha ukali wake katika kufunga mabao, hali hiyo haijamshtua kihivyo mshambuliaji Meddie Kagere wa Simba.

MNIGERIA, Emmanuel Amunike anayekionoa kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars amesema amesikia kilio cha Watanzania wanaotaka kuiona timu yao ikifika mbali katika michuano wanayoshiriki na atapambana kwa kutumia nyota wake kufanikisha hilo.

Amunike alisema anajua Watanzania wamekuwa wakiziangalia timu nyingine zikishiriki mashindano mbalimbali, lakini kwa sasa ni muda wa Stars kufanya mambo kama miaka ya nyuma.

“Mechi dhidi ya Cape Verde itakuwa sio rahisi kwetu hilo linajulikana, ila nimekuwa nikiongea mara kwa mara na wachezaji tuungane na tujitume kuipigania nchi, hakuna jambo zuri kama kuona nyuso ya furaha usoni kwa mtu wako wa karibu na hilo ndio Watanzania wanakihitaji hivi sasa,” alisema Kocha Amunike.

Amunike alifunguka zaidi kwa kusema atatumia mbinu tofauti na alizotumia katika mchezo dhidi ya Uganda ili kuhakikisha anapata matokeo dhidi ya Cape Verde.

Cape Verde itacheza na Stars, Oktoba 12 nchini humo kabla ya kurudiana Oktoba 16 wakiwani tiketi ya Fainali ya Afrika (Afcon 2019) zitakazofanyika Cameroon mwakani.