Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajibu afunguka kuikosa Ndanda, aiweka kiporo Simba

Muktasari:

Nahodha Ajibu hajaichezea Yanga katika michezo mitatu mfululizo alianza dhidi ya Lipuli, Alliance sasa Ndanda jambo lililozua hofu kuwa uenda akawa na tofauti na kocha wake pamoja na kuchochea tetesi za kuhusu kujiunga na Simba,

Dar es Salaam. Nahodha wa Yanga, Ibrahim Ajibu amesema hana tatizo na kocha wake Mwinyi Zahera ila tatizo la nyonga ndio linamsumbua, kuhusu kusajiliwa Simba amesisitiza yeye si msemaji wa hilo  badala yake tungoje mwisho wa msimu.

Nahodha Ajibu hajaichezea Yanga katika michezo mitatu mfululizo alianza dhidi ya Lipuli, Alliance sasa Ndanda jambo lililozua hofu kuwa uenda akawa na tofauti na kocha wake pamoja na kuchochea tetesi za kuhusu kujiunga na Simba,

Ajibu alisema anachukizwa na taarifa zinazosambaa kuwa anashindwa kuungana na timu kutokana na tetesi zinazoendelea za yeye kurudi katika klabu yake ya zamani Simba.

"Unajua mengi yanazungumzwa kuhusiana na mimi kutokuwa pamoja na timu, lakini ukweli unaozungumzwa na viongozi wangu kuwa mimi ni mgojwa huo ndio wa kusikilizwa na sio vinginevyo."

"Nasumbuliwa na nyonga sijafanya mazoezi na timu nitakuaje miongoni mwa nyota wanaosafiri mwalimu na benchi la ufundi wapo sahihi na kauli yangu mimi ni mgonjwa nikipona nitarudi kikosini,"alisema.

Ajibu alitumia nafasi hiyo kuwapongeza nyota wenzake kwa matokeo mazuri waliyopata na kuwaombea heri kuelekea mchezo wao na Ndanda.

TETESI ZA KWENDA SIMBA

"Nina mkataba na timu yangu na nitaendelea kuitumikia na kuhusiana na kusajiliwa Simba naomba nisiwe msemaji wa hilo tukutane mwisho wa msimu,"

"Nipo Yanga naomba kuulizwa kuhusiana na timu yangu hayo mengine tuwaachie wanaotumia karamu zao kujinufaisha wao kwa kuuza magazeti ila kubwa mimi ni mchezaji wa Yanga," alisema Ajibu.