Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kina Bocco, Kagere waliamsha mapema

WAMESHTUKA buana! Nahodha wa Simba, John Bocco Adebayor’, Mnyarwanda Meddie Kagere na Mkenya Francis Kahata ni kama wameshtukia jambo katika kambi ya timu yao iliopo mjini hapa nchini Afrika Kusini na kuamua kuliamsha mapema ili wanoge zaidi.

Nyota hao ambao wote ni washambuliaji wameamua kufanya mazoezi yao binafsi ya kufa mtu kabla ya kuungana na wenzao kwenye gym iliyopo ndani ya kambi yao vizuri inayojiandaa kuingia wiki ya pili tangu ilipoanza Jumatatu iliyopita.

Kagere aliyekuwa Mfungaji Bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 23 na Bocco aliyekuwa mfungaji wa pili ndani ya Simba nyuma ya Kagere kwa mabao yake 16 sambamba na Kahata ingizo jipya Msimbazi, wamekuwa wakifua wenyewe kama njia ya kujiweka fiti zaidi.

Mwanaspoti ambalo linawarushia kitu laivu kutoka Sauzi, lilimshuhudia Bocco akiwa wa kwanza kuingia kwenye mazoezi hayo mapema saa 9:00 alasiri saa za Tanzania, kisha akafuata Kagere akafuata saa 9:15 na baadaye Kahata naye akatimba saa 9:20.

Walipododoswa, sababu ya kufanya hivyo Bocco alisema; “Naenda kwanza gym kujiweka sawa baada ya hapo ndio nitaungana na wenzangu,” alisema Bocco huku akielekea gym.

Pia, Kagere alisema, napenda kuanza mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti, ninapokwenda kuungana na wenzangu nakuwa katika hali nzuri.

Kwa kawaida mazoezi ya pamoja wanaanza saa 10:00 (Tanzania saa 11:00) ambapo Kocha Mkuu Patrick Aussems pamoja na msaidizi wake, Dennis Kitambi hufika uwanjani saa 9:30 kabla ya wachezaji wao kwa ajili ya kuandaa mazingira.