Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sane aingia anga za Liverpool, ishu ya Salah kitendawili

Muktasari:

  • Hivi karibuni Salah alithibitisha kwamba yupo na asilimia nyingi za kuondoka kuliko kubakia kwani hakuna mwafaka wowote uliofikiwa kati yake na mabosi wa Liverpool.

LIVERPOOL imepanga kumsajili winga wa Bayern Munich na Ujerumani, Leroy Sane, 28, katika dirisha lijalo kama mbadala wa mshambuliaji wao raia wa Misri, Mohamed Salah, 32, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Hivi karibuni Salah alithibitisha kwamba yupo na asilimia nyingi za kuondoka kuliko kubakia kwani hakuna mwafaka wowote uliofikiwa kati yake na mabosi wa Liverpool.

Sane ni mmoja kati ya wachezaji wa Bayern waliohusishwa kuondoka katika timu hiyo tangu mwaka jana na mwenyewe alishaweka wazi kwamba bado anatamani kucheza tena England.

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho  wa msimu na hadi sasa hakuna mwafaka wowote uliofikiwa hali inayomweka katika nafasi ya kuondoka bure ama kusaini mkataba wa awali na timu nyingine katika dirisha hili. Tangu kuanza kwa msimu huu Sane amecheza mechi 19 za michuano yote na kufunga mabao matano.


PARIS St-Germain imepanga kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Aston Villa ili kuipata huduma ya mshambuliaji wao raia wa Colombia, Jhon Duran, 21, katika dirisha hili.

Kwa mujibu wa ripoti PSG, imepanga kumtoa mshambuliaji wake Randal Kolo Muani, 26, na pesa kidogo ili kufanikisha dili hilo.

Mkataba wa Duran mwenye umri wa miaka 21, unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


NAPOLI imeanza mazungumzo kwa ajili ya kutaka kumsajili winga wa Liverpool na Italia, Federico Chiesa kwa mkataba wa mkopo wa nusu msimu.

Chiesa mwenye umri wa miaka 27, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Msimu huu amecheza mechi nne za michuano yote na kutoa asisti moja. Hajawa katika ubora wake wa siku za nyuma.


MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Joshua Zirkzee anadaiwa kumwambia wakala wake kwamba anataka kuondoka katika kikosi hicho kwenye dirisha hili kwa ajili ya kutafuta timu itakayompa nafasi kubwa zaidi ya kucheza.

Huduma ya straika huyu mwenye umri wa miaka 23, inawindwa sana na Juventus ambayo inataka kumchukua hata kwa mkopo.


MBALI ya timu za Saudi Arabia na Ulaya, huduma ya mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 27, inawindwa pia na timu za Marekani.

Kwa mujibu wa tovuti ya Teamtalk, Rashford ameingia katika rada za Seattle Sounders inayodaiwa kuwa tayari kumpa mshahara wa zaidi ya Pauni 30 milioni kwa mwaka. Mkataba wake na Man United unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


WOLVES ipo katika hatua za mwisho kumuongeza mkataba mshambuliaji wao raia wa  Brazil, Matheus Cunha licha ya Arsenal kuonyesha nia ya kutaka kumsajili katika dirisha hili.

Cunha mwenye umri wa miaka 25, ni mmoja kati ya mastaa walioonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


MANCHESTER City inajiandaa kuwasilisha ofa nono kwenda Eintracht Frankfurt ili kuipata huduma ya mshambuliaji wa timu hiyo na Misri, Omar Marmoush, 25, ikiwa ni katika mpango wa kuzipiku  Arsenal, Tottenham na Liverpool ambazo zinamhitaji mchezaji huyu pia. Msimu huu Omar amecheza mechi 24 na kufunga mabao 18.


IPSWICH Town imefikia makubaliano ya kumsajili beki wa Atalanta, Ben Godfrey kwa mkopo wa nusu msimu katika dirisha hili. Ben mwenye umri wa miaka 26, anatarajiwa kuwasili England wiki hii kwa ajili ya kukamilisha vipimo vya afya kabla ya kusaini na Ipswich. Staa huyu anaondoka Atalanta kwa sababu hapati nafasi kubwa ya kucheza.