Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sanchez apondwa kwa kiwango duni

Muktasari:

  • Juzi Jumamosi katika mchezo dhidi ya Wolves staa huyo wa kimataifa wa Chile alitolewa uwanjani kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushindwa kuonyesha makali kama ilivyotarajiwa huku United ikiendelea kupata matokeo mabovu.

MANCHESTER United ilimtaka Alexis Sanchez orijino lakini inavyoonekana Arsenal ilifanya utapeli na kuiuzia Sanchez aliye feki.

Ndicho ambacho kinaonekana kwa sasa baada ya mashabiki na wachambuzi kuanza kumshambulia.

Juzi Jumamosi katika mchezo dhidi ya Wolves staa huyo wa kimataifa wa Chile alitolewa uwanjani kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushindwa kuonyesha makali kama ilivyotarajiwa huku United ikiendelea kupata matokeo mabovu.

Na sasa, Sanchez ambaye alichukuliwa katika uhamisho wa kubadilishana na Henrikh Mkhitaryan dirisha la Januari amecheza dakika 831 bila ya kufunga bao lolote katika Ligi Kuu ya England huku bao lake la mwisho likiwa dhidi ya Swansea Machi mwaka huu.

Sanchez ambaye ni staa wa zamani wa Barcelona ndiye mchezaji anayelipwa zaidi United na katika Ligi Kuu ya England akipokea Pauni 350,000 kwa wiki lakini katika kipindi chake cha miezi tisa klabuni hapo ameshindwa kurudia makali aliyokuwa nayo Arsenal.

Mpaka sasa ameifungia United mabao matatu tu katika mechi 22 alizoanza za ligi na anatazamiwa kufikisha miaka 30 Desemba mwaka huu huku kiwango chake kikiwatia wasiwasi mashabiki wa United ambao walishangilia kumnasa pindi timu yao ilipoipiga bao Manchester City katika kuwania saini yake.

“Alexis Sanchez anakaribia kuwa mchezaji mbovu zaidi kusajiliwa na Manchester United baada ya utawala wa Sir Alex Ferguson,” aliandika mwandishi mashuhuri anayeheshimika, John Brewin katika mtandao wake.

Katika Mtandao wa ESPN, Sanchez alipewa alama nne kati ya 10 huku mchambuzi Musa Okwonga akiandika :“Sanchez alikuwa ovyo sana. Alipambana sana lakini alipoteza pasi ovyo, alikuwa anakimbia ovyo tofauti na washambuliaji wenzake.

“Alishindwa kujiweka katika maeneo ya hatari. Kushindwa kwake kuonyesha makali kumeanza kuwa tatizo la msingi.”

Kuchemsha kwa Sanchez ni mwendelezo wa kufanya vibaya kwa wachezaji waliovaa jezi namba 7 Old Trafford miaka ya karibuni.

Kabla yake jezi hiyo ilikuwa inavaliwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Memphis Depay lakini akashindwa kuitendea haki.

Depay kwa sasa amerudisha makali yake katika kikosi cha Lyon ya Ufaransa ambacho katikati ya wiki iliyopita kiliichapa Manchester City katika Ligi ya mabingwa wa Ulaya uwanjani Etihad.

Mchezaji wa mwisho kuitendea haki jezi hiyo alikuwa staa wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye aliirithi jezi hiyo mwaka 2003 kutoka kwa nyota wa England, David Beckham aliyekuwa ametimkia Real Madrid.

Mastaa wengine waliochemsha katika jezi hiyo ni Antonio Valencia ambaye aliamua kuikacha makusudi baadaye huku Angel Di Maria aliyenunuliwa kutoka Real Madrid katika utawala wa Louis van Gaal akichemsha vibaya.

Michael Owen naye aliwahi kupewa jezi hiyo na Sir Alex Ferguson lakini alianza mechi 18 tu za Manchester United katika miaka mitatu aliyokaa klabuni hapo huku mara nyingi zaidi akitokea katika benchi. Hahesabiwi kama aliitendea haki.

Baadhi ya mastaa wengine kando ya Ronaldo ambao waliitendea haki jezi hiyo ni pamoja na mkali wa zamani, George Best ambaye ndiye anaeleweka kama mchezaji wa kwanza kuitendea haki zaidi jezi hiyo na kuipatia umaarufu mkubwa.

Wengine ni nahodha wa zamani Bryan Robson pamoja na mkali wa kimataifa wa Ufaransa.

Eric Canton ambaye naye aliiongezea umaarufu mkubwa kabla hajastaafu soka mwaka 1998 kisha jezi hiyo kwenda kwa Beckham aliyeipa umaarufu mkubwa.