Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Onana bado anaitaka Man Utd, ajipanga kurejea

ONANA Pict

Muktasari:

  • Man United ilimpata Senne Lammens kutoka Royal Antwerp kwa pauni 18 milioni (Sh75.6 bilioni), huku Onana akipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Trabzonspor ya Uturuki.

KIPA Andre Onana, anaendelea kuonyesha azma ya kurejea Man United na kuwa chaguo la kwanza, huku rafiki yake wa karibu akieleza kwamba mambo hayakuwa sawa dhidi ya kocha wa zamani, Ruben Amorim.

Onana, mwenye umri wa miaka 29, alisajiliwa Manchester United kutoka Inter Milan kwa dau la pauni 44 milioni (Sh184.8 bilioni) Julai 2023, lakini hakuwa na maisha mazuri ndani ya klabu hiyo kutokana na kiwango chake kudhoofu, huku akifanya makosa ya mara kwa mara, hali iliyopelekea Amorim kutafuta mbadala katika dirisha la uhamisho msimu uliopita.

Man United ilimpata Senne Lammens kutoka Royal Antwerp kwa pauni 18 milioni (Sh75.6 bilioni), huku Onana akipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Trabzonspor ya Uturuki.

Kipa huyo mchanga wa Ubelgiji, amevutia kwa kiwango kikubwa msimu wake wa kwanza Old Trafford, na utendaji wake katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Everton, Jumatatu, Februari 23, 2026, huku Chris Wheeler wa Daily Mail Sport akimtaja kama msingi wa klabu hiyo kwa muongo mwingine.

Baada ya kuondoka kwa Amorim na Manchester United kuanza kufurahia nguvu mpya chini ya kocha wa muda, Michael Carrick, Onana anaonekana kuwa tayari kupigania nafasi yake tena. Ripoti ya The Guardian wiki hii imedai kuwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 29 anataka kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Man United mara mkopo wake utakapokamilika mwezi Mei 2026.

Rafiki wa kipa huyo, Geremi, amesema hali ya kiakili na kimwili ya Onana, kwa sasa ipo sawa na amekuwa akisisitiza kuwa tayari kurejea Old Traffold, kwa ajili kurejesha utawala wake wa kuwa kipa chaguo la kwanza. 

“Ninamfahamu Onana vizuri na wakati wake akiwa Man United kulikuwa na mambo mengi ambayo hayakuwa sawa. Sio yeye peke yake. Naamini, kwa kuwasili Michael Carrick, mambo yanaonekana kuwa vizuri kwa kila mtu ikiwa ni pamoja na yeye.

“Yeye ana kipaji cha kipekee. Hatua inayofuata ni kurudi Man United na kupigania nafasi yake. Onana daima amekuwa bora anapokabiliana na changamoto. Anafanikiwa anapopewa nafasi ya kuthibitisha uwezo wake,” amesema Geremi.