Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MJIPANGE! Andrea Berta atakavyotumia Pauni 300 milioni kuleta majembe Arsenal

USAJILI Pict

Muktasari:

  • Na kipigo ilichokutana nacho Arsenal uwanjani Emirates mbele ya PSG kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, unaipa hasira timu hiyo kuhakikisha inafanya usajili wa kibeba mwisho wa msimu ili kujenga timu itakayokuwa na uwezo wa kushindania na kubeba mataji makubwa.

LONDON, ENGLAND: ANDREA Berta ameripotiwa kuahidiwa kwamba atakabidhiwa Pauni 300 milioni kwa ajili ya kuzitumia kwenye usajili katika dirisha lake la kwanza la majira ya kiangazi akiwa mkurugenzi wa michezo mpya wa klabu ya Arsenal.

Na kipigo ilichokutana nacho Arsenal uwanjani Emirates mbele ya PSG kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, unaipa hasira timu hiyo kuhakikisha inafanya usajili wa kibeba mwisho wa msimu ili kujenga timu itakayokuwa na uwezo wa kushindania na kubeba mataji makubwa.

Kocha Mikel Arteta alitangaza mapema kwamba dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi litakuwa kubwa kwa Arsenal katika kuhakikisha timu inasajili wachezaji wa maana, ambapo timu hiyo inahitaji kipa namba mbili, beki wa kushoto, kiungo wa mkabaji, winga wa kuchoto na straika na usajili wa mchezaji mwingine wa kuja kumsaidia Bukayo Saka pamoja na kiungo wa kati. Kutokana na hilo, kuna wachezaji hawa saba ambao bosi Berta anaweza kuwanasa kwa mkwanja wake huo wa Pauni 300 milioni ili kufanya Arsenal kuingia msimu ujao wa 2025/2026 ikiwa na kikosi cha kibabe.

USA 01

Joan Garcia (Espanyol): Pauni 25 milioni

Arsenal ilipeleka ofa zao kadhaa kwa Garcia na kukataliwa mwaka jana kabla ya kumchukua kwa mkopo Neto kutoka Bournemouth, lakini bado inahitaji huduma ya mchezaji huyo, ambaye wanaweza kumsajili kwenye dirisha lijalo. Arsenal inahitaji kipa chaguo la pili mwenye uwezo mkubwa ambao atakuja kumpa David Raya wasiwasi wa kupoteza namba yake endapo kama atafanya vibaya uwanjani.

USA 02

Jorrel Hato (Ajax): Pauni 40 milioni

Arsenal inahitaji huduma ya beki wa kushoto mpya, lakini kwa kufanya hivyo itabidi iwafungulie mlango wa kutokea Oleksandr Zinchenko na Kieran Tierney. Hata hivyo, kikosi hicho cha Arsenal kina wachezaji wengi sana wenye uwezo wa kucheza beki ya kushoto ikiwamo Myles Lewis-Skelly, Jurrien Timber, Riccardo Calafiori na Takehiro Tomiyasu, hivyo ujio wa Hato utaongeza ushindani wa namba.

USA 03

Martin Zubimendi (Real Sociedad): Pauni 51 milioni

Huwezi kujihakikishia kwamba kila kitu kipo tayari kuhusu kiungo Zubimendi baada ya kile alichoifanyia Liverpool kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana. Staa huyo alibaki Zubimendi kwenye klabu yake na sasa Arsenal inaripotiwa kuhitaji saini yake na itahakikisha inaipata kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili akacheze sambamba na Mikel Merino huko Emirates.

USA 04

Nico Williams (Athletic Bilbao): Pauni 48 milioni

Arsenal ilianza kumfukuzia staa wa Athletic Bilbao, Nico Williams baada ya kufanya vizuri kwenye fainali za Euro 2024 na kinachoripotiwa ni kwamba kocha Arteta amekuwa akihitaji huduma ya Mhispaniola huyo kwa nguvu zote. Msimu huu, Williams amefanya vizuri kwenye Europa League na hilo litamshawishi Berta kutoa mkwanja kunasa huduma yake akakipige Emirates.

USA 05

Benjamin Sesko (RB Leipzig): Pauni 58 milioni

Kuna imani kubwa kutoka kwa mashabiki wa Arsenal kwamba timu yao ipo kwenye mchakamchaka wa kunasa saini ya straika Viktor Gyokeres wakiamini kwamba gharama yake si kubwa kwa kulinganisha na Alexander Isak. Lakini, Berta hatakuwa tayari kutumia zaidi ya Pauni 100 milioni kwa mchezaji mmoja na ndiyo maana anaweza kuangukia kwa straika Sesko, kijana mwenye uwezo wa kufunga.

USA 06

Jacob Ramsey (Aston Villa): Pauni 50 milioni

Ramsey ni mchezaji sahihi wa kuingia kwenye mipango ya Berta hasa kwa wachezaji wanaomudu vyema kucheza kwenye eneo la kiungo. Uhakika mkubwa kwao ni kwamba Aston Villa inaweza kukubali kumuuza mchezaji huyo ili kuweka sawa vitabu vyao vya hesabu, huku ikiaminika huduma yake itakuwa na faida kubwa endapo kama atanaswa na kwenda kukipiga Emirates msimu ujao.

USA 07

Johan Bakayoko (PSV Eindhoven): Pauni 28 milioni

Wasiwasi wa Bakayoko ni kusumbuliwa na majeraha mara nyingi ambayo yanaweza kumtibulia maisha kama ilivyokuwa kwa Federico Chiesa kwenye Ligi Kuu England akiwa na kikosi cha Liverpool. Bakayoko anatazamwa kama mchezaji mwafaka wa kwenda kumsaidia Bukayo Saka, licha ya kwamba Ethan Nwaneri amekuwa na uwezo mkubwa pia na anacheza kwenye nafasi hiyo ya Saka bila ya shida.