Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabosi wa Real Madrid waweka mtego kwa Van Dijk

Muktasari:

  • Beki huyo Mdachi mwenye umri wa miaka 33, mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na bado haijaeleweka kama ataendelea kukipiga kwenye kikosi hicho cha kocha Arne Slot. 

REAL Madrid inaripotiwa kusikilizia kwa mbali hali ya mambo yanavyoendelea kwa beki wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk na hatima ya mkataba wake.

Beki huyo Mdachi mwenye umri wa miaka 33, mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na bado haijaeleweka kama ataendelea kukipiga kwenye kikosi hicho cha kocha Arne Slot. 

Real Madrid inafahamu hilo na kuripotiwa kwamba bado haijafikia makubaliano kuhusu dili la kumchukua Van Dijk, lakini kinachoelezwa ni kwamba inafuatilia kuona kile inachoweza kufanya kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi endapo kama hatasaini mkataba mpya wa kubaki Anfield.

Van Dijk ni miongoni mwa mastaa watatu wa Liverpool ambao mikataba yao itafika ukomo mwishoni mwa msimu huu sambamba na Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold.


Jamie Bynoe-Gittens

ARSENAL imeripotiwa kupiga hatua nzuri kwenye mchakamchaka wa kuwania huduma ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Jamie Bynoe-Gittens katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anatarajia kufungua pochi kunasa mshambuliaji mpya dirisha lijalo baada ya kushindwa kufanya hivyo usajili wa dirisha la Januari. Arsenal inahitaji straika kwa nguvu zote.


Sverre Nypan

MANCHESTER City imeripotiwa kuwa na matumaini ya kuzipiku Arsenal na Liverpool kwenye mbio za kufukuzia huduma ya staa wa Norway, Sverre Nypan. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18 anatajwa kama mmoja wa wachezaji makinda wenye vipaji vikubwa wanaoibukia kwenye soka kwa sasa kutokana na kufanya vizuri kwenye kikosi cha Rosenborg. Nypan alicheza mechi yake ya kwanza kikosi cha wakubwa 2022.


Ibrahima Konate

PARIS Saint-Germain na Real Madrid zimeripotiwa kwamba zitaingia kwenye vita ya kumfukuzia huduma ya beki wa kati wa Liverpool, Ibrahima Konate. Liverpool msimu huu imekuwa kwenye kiwango bora licha ya mastaa watatu kutofahamika hatima zao kutokana na mikataba kufika tamati mwishoni mwa msimu. Lakini, sasa mambo yanaweza kuwa magumu zaidi baada ya Konate naye kuwa kwenye rada za vigogo.


Ademola Lookman

MANCHESTER United imeripotiwa kwamba itaingia kwenye vita na Newcastle United kufukuzia saini ya mshambuliaji wa Kinigeria, Ademola Lookman. Staa huyo amekuwa kwenye kiwango matata huko Atalanta ya Italia akitamba chini ya kocha Gian Piero Gasperini. Ubora wake umezifanya klabu za Ligi Kuu England kutaka kumrudisha mshambuliaji huyo akacheze huko baada ya kuibukia Everton.


Kevin de Bruyne

KIUNGO wa kimataifa wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne anaripotiwa kuwasikilizia Manchester City wafanye uamuzi kama wanataka waendelee msimu ujao au wataachana naye kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi wakati mkataba wake utakapofika tamati huko Etihad. De Bruyne, 33, atakubali kuwa mchezaji wa mechi chache endapo atabaki Man City kwa kusaini dili jipya.


Paul Pogba

KIUNGO wa Ufaransa, Paul Pogba anaripotiwa kuwa kwenye mipango ya kujiunga na Inter Miami ya Marekani wakati adhabu yake ya kufungiwa itakapofika ukomo mwezi ujao. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Juventus, Novemba mwaka jana.


Castello Lukeba

REAL Madrid inajiandaa kufukuzia huduma ya beki wa kati wa RB Leipzig, Castello Lukeba dirisha lijalo la majira ya kiangazi huko Ulaya. Beki huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 22 amekuwa kwenye rada za Liverpool, Chelsea na Manchester United zikimtaka akakipige kwenye Ligi Kuu England. Madrid inaamini itakuwa kwenye mikono salama ikinasa saini ya Lukeba.