Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Al Hilal ataka Mo Salah aletwe fasta

Tetesi Pict

Muktasari:

  • Salah mwenye umri wa miaka 32, mkataba wake unatarajiwa kualizika mwisho wa msimu huu na hadi sasa Liverpool haijafanya naye makubaliano yoyote ya kusaini mkataba mpya.

KOCHA wa Al-Hilal, Jorge Jesus amewaambia mabosi wa timu hiyo anahitaji huduma ya mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah dirisha lijalo la majira ya kiangazi na amesisitiza anaendana kabisa na mifumo yake.

Salah mwenye umri wa miaka 32, mkataba wake unatarajiwa kualizika mwisho wa msimu huu na hadi sasa Liverpool haijafanya naye makubaliano yoyote ya kusaini mkataba mpya.

Msimu huu Salah amekuwa katika kiwango bora akifunga mabao 26 na kutoa asisti 18 akiisaidia Liverpool kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa muda mrefu.

Mabosi wa Al-Hilal wanamuangalia Salah kama mbadala sahihi wa Neymar Jr ambaye aliondoka Januari mwaka huu baada ya kutofikia matarajio waliyoyaweka kwake.


Darwin Nunez

MABOSI wa Liverpool wamesisitiza straika wao kutoka Uruguay, Darwin Nunez, 25, hatouzwa hivi sasa licha ya kupokea ofa nono kutoka kwa matajiri wa Saudi Arabia na anahitajika na Al Nassr. Inaelezwa waarabu hao waliweka mezani zaidi ya Pauni 150 milioni kama ada ya uhamisho kwa ajili ya staa huyo ambaye msimu huu amecheza mechi 33 za michuano yote, amefunga mabao sita na kutoa asisti tano.


Nico Williams

ARSENAL ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao na timu ya taifa ya Hispania, Nico Williams, 22, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Nico ambaye ameonyesha kiwango bora akiwa na timi ya taifa ya Hispania katika michuano ya Euro awali alipewa nafasi kubwa zaidi ya kutua Barcelona lakini inaonekana kuwa ngumu kwa timu hiyo kukamilisha uhamisho wake kutokana na hali yao ya kiuchumi.


Adam Wharton

MANCHESTER City imeendelea kumfuatilia kwa karibu kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton ambaye inataka kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mchakato wa kumfuatilia ulikwama kwa muda baada ya staa huyu wa kimataifa wa England kupata majeraha lakini sasa maskauti wa mabingwa hao watetezi wamerudi kazini na wanatarajia atakubali kujiunga nao msimu ujao.


Trent Alexander-Arnold

BAADA ya kusisitisha mchakato kwa muda, mabosi wa Real Madrid wameanza tena harakati zao za kutaka kumsajili  beki wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Trent mwenye umri wa miaka 26, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na amekuwa katika rada za Madrid tangu mwaka jana. Msimu huu amecheza mechi 32 za michuano yote na kutoa asisti saba.


Jamie Gittens

Borussia Dortmund inahitaji kati ya Pauni 66 hadi 83 milioni ili kumuuza winga wao raia wa England, Jamie Gittens ambaye amekuwa akiwindwa na Chelsea na Bayern Munich. Timu zote hizi zinahitaji saini ya staa huyu katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kujaribu kumsajili mwezi uliopita wa dirisha dogo na Dortmund ikagona kumuuza.


Jean-Philippe Mateta

MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, 27, ameendelea kuzivutia timu nyingi zaidi, huku  Olympique Lyon na Atletico Madrid nazi zikitajwa. Mateta mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu na timu nyingi katika foleni ya kutaka huduma yake kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu.


Florian Wirtz

LICHA ya Bayer Leverkusen kudaiwa ipo kwenye hatua nzuri ya kumsainisha mkataba mpya kiungo wao, Florian Wirtz, kocha wa Manchester City, Pep Guardiola bado ana matumaini na shauku ya kuipata huduma ya staa huyo dirsha lijalo. Inaelezwa Leverkusen ipo tayari kumuuza Wirtz mwisho wa msimu huu lakini wanataka kumsainisha mkataba mpya kwanza ili wamuuze kwa pesa nyingi.