Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jina la Alexander Isak sasa latua kwa vigogo wa PSG

Muktasari:

  • Isak ambaye ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Newcastle ameivutia sana PSG kwa kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge na Newcastle hususani msimu huu ambapo amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga mabao 11.

PARIS St-Germain ipo tayari kulipa Euro 100 milioni ili kumsajili straika wa Newcastle United na Sweden, Alexander Isak, 25, katika dirisha lijalo ili kuboresha safu yao ya ushambiluaji.

Isak ambaye ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Newcastle ameivutia sana PSG kwa kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge na Newcastle hususani msimu huu ambapo amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga mabao 11. Ikiwa PSG itafanikiwa kuipata saini ya fundi huyu litakuwa ni pigo kubwa kwa Arsenal iliyotajwa kutaka kumsajili tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana.

Kwa mujibu wa ripoti, Newcastle inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 100 milioni ili kumuuza fundu huyu ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028.


MPANGO wa Liverpool kutaka kumsajili mshambuliaji wa Brighton na Brazil, Joao Pedro katika dirisha la majira ya baridi mwakani huenda ukafeli kwa sababu Brighton haitaki kumuuza mchezaji huyo wakati huo badala yake inataka kuendelea kuwa naye hadi mwisho wa msimu.

Staa huyu mwenye umri wa miaka 23, ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi hicho.


MABOSI wa  PSG wanataka kulipa Euro 58 milioni kwenda Athletic Bilbao kwa ajili ya kuvunja mkataba wa winga wa timu hiyo na Hispania, Nico Williams, 22, katika dirisha lijalo.

Mkataba wa Nico una kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa kiasi hicho cha pesa lakini kwa sasa Manchester United na Barcelona  pia zinahitaji kumsajili hali inayoweza kusababishwa auzwe kwa pesa nyingi.


BARCELONA ipo tayari kumwachia kiungo wao raia wa Uholanzi, Frenkie de Jong katika dirisha lijalo la majira ya baridi au kiangazi.

De Jong anahusishwa kuondoka baada ya mashabiki kutokuwa na imani naye na mara kadhaa amekuwa akizomewa anapoingia uwanjani.

Kiungo aliwahi kuhusishwa sana na Manchester United katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.


NEWCASTLE ni miongoni kwa timu zinazohitaji saini ya beki kisiki wa Barcelona, Eric Garcia, 23, katika dirisha la majira ya baridi mwakani.

Hata hivyo, Garcia ambaye kwa sasa sio mmoja kati ya wachezaji wanaopata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha Barca, haonekani kuwa na mpango wa kutaka kuondoka na anataka kubakia ili kupambania nafasi yake katika viunga hivyo.


WINGA wa Barcelona na Hispania,  Lamine Yamal, 17, yupo katika hatua za mwisho kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye timu hiyo hadi mwaka 2030.

Mkataba wa sasa wa Yamal unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 na inataka kumsainisha mkataba huo mpya mapema kwa sababu timu kubwa nyingine zimeshaanza harakati za kutaka kumsajili.


MABOSI wa Newcastle wamepanga kumruhusu straika wao raia wa England, Callum Wilson, 32, kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi wakati ambao mkataba wake utakuwa umeisha. Wilson hapati nafasi ya kutosha kikosini hali inayosababisha vigogo wa klabu hiyo wasimpe ofa ya mkataba mpya.


WINGA wa Arsenal, Reiss Nelson ana nafasi kubwa ya kusaini mkataba wa kudumu wa kuendelea kusalia Fulham baada ya Arsenal kumpa ruhusa ya kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa atapata timu itakayokuwa tayari kumnunua jumla. Alitua Fulham ili kucheza kwani hayupo katika mipango ya Mikel Arteta.