Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland avunja rekodi ya Messi Ligi ya Mabingwa Ulaya

HALAAND Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefikisha mabao 60 kwa haraka zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya PSG katika mchezo uliochezwa jana Jumatano, Oktoba 14, 2026.

MANCHESTER. ENGLAND: Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefikisha mabao 60 kwa haraka zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya PSG katika mchezo uliochezwa jana Jumatano, Oktoba 14, 2026.

Haaland amefikisha mabao 61 katika mechi 60 alizocheza kwenye mashindano hayo na hivyo kumpiku Lionel Messi, ambaye alifikisha mabao 60 baada ya kucheza mechi 80.

Rekodi hiyo imeendeleza historia ya mshambuliaji huyo  wa Norway ambaye amekuwa akivunja rekodi mbalimbali za ufungaji tangu alipoanza kucheza Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu ya RedBull Salzburg ya Austria.

Wakati Haaland akiweka rekodi hiyo, mshambuliaji Robert Lewandowski alihitaji mechi 85, Kylian Mbappé alitumia mechi 89 na Cristiano Ronaldo alitumia mechi 98 kufikia idadi hiyo.

Kwa upande wa umri, Haaland pia amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikisha mabao 60 katika mashindano hayo, akiwa na miaka 26 na siku 85. Amempita Messi kwa tofauti ya siku moja, kwani nyota huyo wa Argentina alikuwa na miaka 26 na siku 86 alipofikia hatua hiyo.

Haaland pia amevunja rekodi nyingine ndani ya kikosi cha Man City, baada ya kufikisha mabao 38, akimpiku Sergio Aguero aliyekuwa akishikilia rekodi ya mabao 26, katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Rekodi hiyo imekuja wakati Manchester City ikipoteza mchezo huo kwa mabao 4-2 dhidi ya PSG, licha ya Haaland kuifungia timu yake mabao yote mawili katika kipindi cha pili baada ya wenyeji kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 3-0.

Mshambuliaji huyo alianza kufunga katika dakika ya 53, kisha kuongeza bao la pili katika dakika ya 75, akionyesha uwezo wake wa kutumia nafasi licha ya timu yake kuwa katika mazingira magumu dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, mabao hayo hayakuweza kuizuia Man City kupoteza mchezo huo, kwani PSG ilipata mabao kupitia Désiré Doué, Ousmane Dembélé, Vitinha na Maghnes Akliouche.

Kwa rekodi hiyo mpya, Haaland ameendelea kujitengenezea nafasi miongoni mwa wafungaji bora wa kizazi chake katika soka la Ulaya, huku akikaribia hatua nyingine kubwa ya kufikisha mabao 70 katika mashindano hayo.

Kwa sasa, rekodi ya kufikisha mabao 70 kwa mechi chache zaidi inashikiliwa na Messi, aliyehitaji mechi 90.