Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Galatasaray wahaha kwa Osimhen, Waarabu watajwa

Muktasari:

  • Osimhen, 26, ambaye anacheza kwa mkopo wa msimu mmoja Galatasaray, mkataba wake na Napoli unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

NAPOLI imekataa ofa ya Euro 65 milioni kutoka Galatasaray inayohitaji kumsajili straika wao raia wa Nigeria, Victor Osimhen dirisha hili.

Osimhen, 26, ambaye anacheza kwa mkopo wa msimu mmoja Galatasaray, mkataba wake na Napoli unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

Mbali ya Galatasaray, timu nyingi zimeonyesha nia ya kumsajili fundi huyu, ingawa kuna zile zinazopewa nafasi kubwa ya kumpata ikiwemo Manchester United na Arsenal.

Mbali ya timu za Ulaya, Osimhen pia ana ofa kibao kutoka Saudi Arabia ambako amewekewa ofa nono ya mshahara unaofikia Pauni 40 milioni kwa msimu.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Osimhen amecheza mechi 20 za michuano yote, akafunga mabao 16 na kutoa asisti tano.


AJAX imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Barcelona raia waHispania, Ansu Fati, 22, katika dirisha hili la majira ya baridi baada ya timu yake kuweka wazi ipo tayari kumuuza. Ansu Fati ambaye mkataba wake na Barca unamalizika mwaka 2027,  anahusishwa kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha wababe hao wa Hispania. Kuna kila dalili akaondoka dirisha hili na klabu kadhaa kubwa zinamtaka.


STRAIKA wa Aston Villa na timu ya taifa ya Colombia, Jhon Duran, 21, anadaiwa kuwa alifanya vipimo jana ikiwa ni katika hatua za kukamilisha mchakato wa kujiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia ambayo imeweka mezani kiasi kinachodaiwa kufikia Euro 77 milioni kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili. Duran anawindwa sana na Al Nassr kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu na anaenda kuungana na Cristiano Ronaldo kwenye safu ya umaliziaji.


ARSENAL inatarajiwa kutuma ofa ya pili nono kwenda kwa Aston Villa ili kuipata saini ya straika wa timu hiyo na timu ya taifa ya England, Ollie Watkins, 29, kabla ya dirisha hili la majira ya baridi kufungwa. Watkins ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao 11.


MANCHESTER United ipo katika mazungumzo mazito na Barcelona juu ya mshambuliaji wao raia wa England, Marcus Rashford, 27, ambaye inahitaji kumsajili katika dirisha hili. Licha ya Man United kuwa tayari kumuuza na Rashford mwenyewe kuwa tayari kufanya hivyo, inaonekana kuna asilimia chache za dili hilo kukamilika kabla ya dirisha kufungwa Jumatatu ya wiki ijayo.


Napoli inaendelea kupambana kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Karim Adeyemi, 23, katika dirisha hili lakini inakumbana na changamoto ya kufikia makubaliano juu ya ada ya uhamisho. Adeyemi ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu huu amecheza mechi 14 za michuano yote na kufunga mabao matano.


Napoli wamewaambia wawakilishi wa winga wa Manchester United, Alejandro Garnacho, 20, watajaribu tena kumsajili fundi huyu ikiwa bei yake itashuka. Inaelezwa mashetani hao wekundu wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 70 milioni ili kumuuza staa huyo na hawatoshusha bei yake jambo ambalo limewaondoa Man United kwenye mchakato huo.


EVERTON inakaribia kufikia makubaliano ya kumrudisha straika wa Chelsea, Armando Broja dirisha hili na inadaiwa wanataka kufanya hivyo ili kuchukua mchezaji mwingine kwa mkopo kutoka kwa matajiri hao wa Darajani. Broja hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa tangu atue Everton kwa mkopo katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.