Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dortmund yajiweka kando kufukuzia saini ya Sancho

TETESI Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alipata umaarufu akiwa na Dortmund kabla ya kujiunga na Manchester United kwa Pauni milioni 73 mwaka 2021, lakini alipitia wakati mgumu Old Trafford na hatimaye kuingia kwenye mgogoro na aliyekuwa kocha wa United, Erik ten Hag.

BORUSSIA Dortmund haina nia ya kumsajili Jadon Sancho katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, huku mustakabali wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England ukiwa haueleweki.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alipata umaarufu akiwa na Dortmund kabla ya kujiunga na Manchester United kwa Pauni milioni 73 mwaka 2021, lakini alipitia wakati mgumu Old Trafford na hatimaye kuingia kwenye mgogoro na aliyekuwa kocha wa United, Erik ten Hag.

Sancho alirejea Dortmund kwa mkopo katika nusu ya pili ya msimu uliopita, na kwa kiasi kikubwa aliisaidia timu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, United bado ilikuwa na nia ya kumuuza majira ya joto yaliyopita, na hatimaye ikamruhusu ajiunge na Chelsea kwa mkopo.

Mkataba na Chelsea una kipengele cha kumsajili kwa Pauni 25 milioni mwishoni mwa msimu huu, huku ikitakiwa kulipa Pauni milioni tano kuepuka kumsajili. Licha ya kuonyesha ubora mara kadhaa, mustakabali wake bado haupo wazi. Mkataba wake Man U unaisha 2026.


Douglas Luiz

JUVENTUS iko tayari kumtoa kiungo Douglas Luiz, 27, kwa Manchester United kama sehemu ya ofa kwa ajili ya mshambuliaji Rasmus Hojlund mkataba wake unamalizika 2029. Pia, Juventus inaonyesha nia ya kumsajili winga wa Manchester United, Antony, lakini klabu hiyo ya Serie A haitakuwa tayari kulipa dau la Pauni 42.4 milioni zinazohitajika kumsajili mchezaji huyo anayekipiga Real Betis kwa mkopo.


Leny Yoro

LENY Yoro, 19, anajutia kujiunga na Manchester United badala ya Real Madrid majira ya kiangazi yaliyopita, na sasa amemtaka wakala wake amsaidie kujiunga na klabu hiyo ya Hispania kwa msimu ujao. Manchester United haina mpango wa kumuuza beki huyo na iwapo italazimika kukubali kufanya hivyo, itataka kupata faida juu ya Pauni 50.9 milioni ilizolipa kumsajili dirisha kubwa lililopita. Mkataba wa Yoro Old Trafford unamalizika 2029.


Liam Delap

ARSENAL imewasiliana na wakala wa mshambuliaji wa Ipswich Town, Liam Delap, 22, ambaye pia anawaniwa na Chelsea na Manchester United. Straika huyo ambaye chama lake limeshuka daraja msimu huu, amekuwa akiwaniwa na timu kibao zikiwamo za Hispania, huku ikielezwa uhakika wa kubaki Ipswich msimu ujao ni mdogo. Mkataba wake unamalizika 2029.


Mason Greenwood

MSHAMBULIAJI wa Marseille na England, Mason Greenwood, 23, ameingia anga za Liverpool inayofuatilia kwa karibu maisha yake Ufaransa ili kuwasilisha ofa kabla ya dirisha la majira ya kiangazi halijafunguliwa. Katika mkataba wake unaomalizika 2029 huko Marseille, Greenwood anauzwa Pauni 59.3 milioni Msimu huu amecheza mechi 32 na kufunga mabao 18, akitoa asisti tano.


Jake Evans

MANCHESTER United na Tottenham Hotspur zinajiandaa kuwasilisha ofa za Pauni 12.7 milioni ili kumnasa mshambuliaji chipukizi wa Leicester City na England, Jake Evans, 16, baada ya kucheza mechi yake ya kwanza kwenye Ligi Kuu England. Mkataba wake Leicester City unamalizika 2030. Pia Tottenham inaonyesha nia ya kumsajili winga wa Liverpool, Federico Chiesa ambaye anaweza kupatikana kwa Pauni 15 milioni.


Gianluigi Donnarumma

KIPA wa PSG, Gianluigi Donnarumma ameziingiza vitani Bayern Munich, Manchester City na Juventus zinazodaiwa kuweka mzigo mezani zikimtaka msimu ujao. Hata hivyo, Inter pia inadaiwa kuja kwa kasi ikiwa na ofa nzuri. Donnarumma aliyeiwezesha Inter kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, waajiri wake pia wanataka kumuongezea mkataba.


Vanja Milinkovic-Savic

MANCHESTER United imerudi kwa kipa wake wa zamani na Hispania, Vanja Milinkovic-Savic, 28, anayekipiga Torino. Mchezaji huyo ambaye pia anawaniwa na Manchester City ana kipengele cha kuondoka kwa cha dau la Pauni 17 milioni ambacho Torino inatarajiwa kukipandisha kupitia mkataba mpya iliomuandalia kabla ya msimu kumalizika. Mkataba wa sasa unamalizika 2026.