Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Davies akubali kusaini mkataba wa awali Madrid

Muktasari:

  • Davies mwenye umri wa miaka 24, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na amepewa ofa ya mkataba mpya na Bayern Munich, lakini amekataa kwa kile kinachoelezwa kwamba ameshafanya makubaliano na Madrid.

BEKI wa pembeni wa Bayern Munich na Canada, Alphonso Davies, 24, yupo tayari kusaini mkataba wa awali ili kuichezea Real Madrid katika dirisha la majira ya baridi mwakani na inaelezwa tayari ameshafikia makubaliano na mabosi wa timu hiyo.

Davies mwenye umri wa miaka 24, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na amepewa ofa ya mkataba mpya na Bayern Munich, lakini amekataa kwa kile kinachoelezwa kwamba ameshafanya makubaliano na Madrid.

Real Madrid imekuwa katika mazungumzo na beki huyo wa kimataifa wa Canada kwa muda mrefu na imeripotiwa kwamba imeshafikia makubaliano ya kumsajili.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 15 za michuano yote na kutoa asisti tatu.


Leon Goretzka

MANCHESTER United inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Union Berlin katika dili la kuwania saini ya kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka ambaye anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Goretzka mwenye umri wa miaka 29, msimu huu amecheza mechi tisa za michuano yote. mkataba wake unamalizika 2026.


Igor Jesus

FULHAM imeungana na Brentford kwenye vita ya kuwania saini ya straika wa Botafogo na Brazil, Igor Jesus, 23, katika dirisha lijalo ambapo itatakiwa kushinda vita pia mbele ya Newcastle United na Nottingham Forest ambazo pia zinahitaji huduma yake. Tangu kuanza kwa msimu huu Igor amecheza mechi 24 za michuano yote na mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027.


Joachim Andersen

JUVENTUS ipo katika mchakato wa kuboresha eneo la ulinzi na imepanga kusajili mabeki wawili katika dirisha lijalo ikiwa pamoja na Joachim Andersen kutoka Fulham na wa Chelsea, Mfaransa  Benoit Badiashile, 23. Mastaa hao wanaweza kuigharimu Juventus zaidi ya Pauni 50 milioni ikiwa itataka kuwasajili jumla, lakini taarifa zinaeleza kwamba inawataka kwa mkopo.


Tariq Lamptey

WEST Ham United inataka kuipiku Tottenham Hotspur katika vita ya kuwania saini ya beki wa kulia wa Brighton, Tariq Lamptey, 24, ambaye pia anawindwa na Everton. Lamptey ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, tangu msimu huu uanze amecheza mechi nne za michuano yote na kutoa asisti moja.


Jonathan David

MAZUNGUMZO kati ya mabosi wa Bayern Munich na wawakilishi wa mshambuliaji wa Lille na Canada, Jonathan David, 24, yameripotiwa kufikia hatua nzuri. Mkataba wa Jonathan unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na tayari ameshafanya uamuzi wa kuondoka licha ya kupewa ofa ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Lille, lakini amekataa.


Mats Hummels

BEKI wa AS Roma na Ujerumani, Mats Hummels, 35, anafikiria kustaafu kucheza soka Januari mwakani ikiwa hatapata timu ya kujiunga nayo. Hummels anataka kuondoka Roma katika dirisha  lijalo kwa sababu hapati nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha wababe hao. Msimu huu amecheza mechi moja pekee tangu ulipoanza.


Khvicha Kvaratskhelia

BARCELONA ipo tayari kutoa Pauni 67 milioni kwa ajili ya kumnunua winga wa Napoli na Georgia, Khvicha Kvaratskhelia katika dirisha la majira ya baridi mara tu likapofunguliwa Januari, 2025. Khvicha mwenye umri wa miaka 23, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027. Msimu huu amecheza mechi 14 za michuano yote.