Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Appiah: Nikiongea kitu kuhusu soka la Ghana, wataniua!

Muktasari:

  • Na kama hilo halitoshi, pigo jingine kwa taifa hilo ni ukweli kwamba kocha Kwesi Appiah, ambaye alifukuzwa kazi ya kuifundisha Ghana baada ya kutolewa katika hatua ya 16-Bora ya Afcon 2019 kule nchini Misri, ameiwezesha Sudan, iliyoathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kufuzu ushiriki wa fainali zijazo za Afcon 2025.

MSHITUKO mkubwa katika kampeni zilizomalizika jana za kuwania kufuzu ushiriki wa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 ni kushindwa kufuzu kwa mabingwa mara nne wa michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya kitaifa barani Afrika, Ghana.

Kama hilo halitoshi, pigo jingine kwa taifa hilo ni ukweli kwamba kocha Kwesi Appiah, ambaye alifutwa kazi ya kuifundisha Ghana baada ya kutolewa katika hatua ya 16-Bora ya Afcon 2019 kule nchini Misri, ameiwezesha Sudan iliyoathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe, kufuzu ushiriki wa fainali zijazo za Afcon 2025.

Mwanaspoti lilimuuliza Appiah kuhusu wanayopitia Ghana hivi sasa ambapo alijibu kwa kifupi tu: "Nikizungumza wataniua."

Wakati wa mechi hizo za kufuzu, Ghana na Sudan zilipangwa katika kundi moja la F, zilipokutana kule Ghana zilitoka 0-0 na marudiano Sudan ikashinda 2-0, huku Appiah akiwaongoza Wasudan kulizamisha taifa lake lililomfukuza kazi ya ukocha.

Kinachouma ni kwamba, tangu Ghana mara ya mwisho ilipofikishwa hatua ya 16-Bora na Appiah, haijapata mafanikio mengine. Katika fainali za 2021 na 2023 ilitolewa hatua ya makundi kabla ya kushindwa kufuzu kwa fainali zijazo za 2025.

Katika Kundi F la kufuzu kwa fainali za 2025, Angola imemaliza kileleni ikiwa na pointi 14 (imeshinda 4, sare 2, vipigo 0), ikiftaiwa na Sudan iliyokusanya pointi 8 (imeshinda 2, sare 2, vipigo 2) wakati Niger ikimaliza ya tatu na pointi 7 (imeshinda 2, sare 1, vipigo 3) huku Ghana ikiburuza mkia na pointi 3 (imeshinda 0, sare 3, vipigo 3).

Appiah alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Ghana kuanzia Aprili 4, 2017 hadi alipofutwa kazi Januari 4, 2020.

Timu ya taifa ya Ghana maarufu kama 'The Black Stars' imetwaa taji la Afcon mara nne; 1963, 1965, 1978 na 1982, ikizidiwa na mataifa mawili tu Cameroon (5) na Misri (7).