Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkenya Pamba Jiji ataja mambo matano

BARAZA Pict

Muktasari:

  • Baraza ametoa tahadhari hiyo baada ya kikosi hicho kupata sare ya bao 1-1 mbele ya  Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kuiwezesha timu hiyo kukaa kileleni kwa muda ikiitoa Mbeya City.

PAMBA Jiji imeonja utamu wa kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa saa mbili na ushei kabla ya kushushwa na Simba, huku kocha Francis Baraza akiwapa ujanja mastaa wa timu hiyo akitaja mambo matano watakayokomaa nao kabla ya kurudi uwanjani.

Baraza ametoa tahadhari hiyo baada ya kikosi hicho kupata sare ya bao 1-1 mbele ya  Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kuiwezesha timu hiyo kukaa kileleni kwa muda ikiitoa Mbeya City.

Pamba imefikisha pointi tisa na kuishusha Mbeya City yenye nane, lakini mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya Muungano, ilikaa kwa saa chache kabla ya kushushwa na Simba iliyoifumua JKT Tanzania kwa mabao 2-1 na kutofautiana uwiano wa mabao tu.

Hata hjivyo Pamba imecheza mechi sita, wakati Simba imeshuka uwanjani mara tatu licha ya kila mmoja kuwa na pointi tisa na kocha Baraza pamoja na kuwapongeza wachezaji kwa kupambana na kupata sare mbele ya Singida Black Stars ambayo haijapoteza katika mechi 12 mfululizo, alisisitiza wanapaswa kuongeza bidii maradufu.

BARA 01

“Nawapongeza vijana wangu kwa juhudi walizozifanya na wamecheza mpira mzuri kulinganisha na mechi zote tulizozicheza,” amesema Baraza na kuongeza;

“Jambo la msingi hapa ni mwendelezo tu maana kama wamecheza namna hii wasibweteke wawe na mwendelezo na kuona tunaweza kufanya vizuri katika michezo inayokuja.”

Kocha huyo raia wa Kenya amesema katika mechi hiyo wachezaji walitimiza kwa asilimia 60 maelekezo aliyowapatia kwa kufanya kile alichowaeleza katika uwanja wa mazoezi.

Amesema anaridhishwa na namna wanavyotimiza vizuri maelekezo yake, huku akitaja kuongeza juhudi, kuwapa motisha, kuwainua na kufanya mazoezi kwa bidii kama silaha ya kuwafanya waendelee kuwa tishio Ligi Kuu.

BARA 02
BARA 02

“Nasisitiza vijana wangu wasibweteke kwa sababu ligi ni mbio ndefu, wazidi tu kusukuma tuone mwisho wa ligi tunamaliza wapi. Muhimu ni kuzoa pointi mkondo wa kwanza ili mzunguko wa pili upige hesabu zako,” amesema.

Akizungumzia kurejea kwa kipa namba moja, Yona Amosi baada ya majeraha ya muda mrefu, Baraza alimpongeza kwani ni tegemeo kwa timu hiyo, hivyo uwepo wake utawaongezea nguvu kikosini.

“Ni kipa ambaye nimemkosa kwa mechi nyingi na alikuwa ni pigo kwetu kama timu kwa sababu jeraha lake limemchukua muda mwingi kupona. Namsihi aongeze zaidi ya kile alichokifanya leo na tumkemee shetani asipatwe tena na majeraha aliyokuwa nayo,” amesema kocha huyo.