Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Msauzi’ aongeza dozi Yanga, mastaa wa kigeni waongezeka!

YANGA Pict


YANGA hivi sasa inaendelea kujiandaa na msimu wa 2026-2027 chini ya benchi jipya la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu, Manqoba Mngqithi.


Lakini, unaambiwa huko mazoezini kumepamba moto kwani kocha huyo raia wa Afrika Kusini ameongeza dozi ya tizi, huku wachezaji wanne wa kigeni wakitua fasta kuanza kukiwasha.


Kikosi hicho kilianza kujinoa Julai 23, 2026 kwa ajili ya kuianza safari ya kusaka mafanikio msimu ujao, lakini kiliwakosa baadhi ya wachezaji ambao walikwenda makwao kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Lakini, jambo zuri ni kwamba, taratibu kikosi hicho kinaanza kukamilika kwani winga Maxi Nzengeli, beki Chadrack Boka, kiungo Duke Abuya na mshambuliaji Laurindo Aurélio ‘Depu’ wametua kuungana na wenzao.

Mmoja kati ya wachezaji wa Yanga, aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Wachezaji wa kigeni wengi walikuwa nje ya kambi, lakini kuanzia wiki hii inayoanza leo (jana) wataanza kuingia mazoezi, nimemuona Maxi, Boka na wengine waliokuwa nje ya Tanzania.”

KOCH 03

MSAUZI AMEBADILI DOZI

Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zinabainisha kwamba, kocha Manqoba amewabadilishia dozi mastaa wa Yanga huku akiachana na ratiba ya mazoezi ya masaa matatu kwa siku.

Yanga ilipoianza safari hiyo ya pre-season, kocha huyo alianza na dozi ya mazoezi ya mara moja pekee yakifanyika asubuhi, lakini kuanzia wiki hii rasmi kikosi hicho kitakuwa kikijinoa mara mbili, asubuhi na jioni.

“Kocha ameongeza dozi kwa wachezaji, sasa watakuwa wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni na wachezaji wanasema mazoezi ya mwalimu huyo ni magumu lakini ni ya kisasa, unakimbia sana lakini na mpira unacheza.”

KOCH 02

HABARI NJEMA

Kwa mashabiki wa Yanga, habari njema kwao ni kwamba, beki Dickson Job amerejea baada ya kukaa nje miezi minne kutokana na kupata jeraha la goti kwenye mechi ya Kariakoo Dabi iliyochezwa Machi 1, 2026, Zanzibar. 

Lakini pia mshambuliaji Clement Mzize naye amerejea baada ya kukaa nje takribani msimu mzima baada ya kujitonesha jeraha la goti akiwa mazoezini, jambo lilisababisha afanyiwe upasuaji wa pili, uliomuweka nje kwa miezi mitano.

Taarifa za ndani zilisema kuwa: “Wachezaji hao wamerejea mazoezini, huku wote wakiendelea kujinoa chini ya uangalizi wa madaktari ambao wanaendelea kuangalia hali zao kwa ukaribu ili wasiharakishe kuwarudisha uwanjani.”