Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yajiandaa kumalizana na Alliance

Mwanza.Baada ya kuwasili jijini hapa timu ya Yanga jana imefanya mazoezi yake kwa ajili ya kujiweka fiti na mchezo wao ujao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Alliance.

Wakijifua chini ya Kocha wao Mwinyi Zahera kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba, nyota wa kikosi hicho,wameonekana kuwa na ushirikiano haswa katika kupasiana mipira na kufunga.

Mazoezi yaliyofanyika leo ni pamoja na wachezaji kuchengana ili kupata pumzi, kupigiana pasi na kufunga.

Hata hivyo, mashabiki nao hawakuwa mbali,kwani walihakikisha wanashuhudia matizi hayo

mwanzo mwisho.

Akizungumza baada ya kuwasili jijini hapa,Zahera alisema kuwa kutokana na umuhimu wa mchezo huo,hawaoni cha kupoteza badala yake dhamira yao ni kutinga Nusu Fainali.

Alisema kuwa anawafahamu sana wapinzani wao walivyo na ushindani,hivyo maandalizi yao yatakuwa vizuri ili kufikia malengo yao na kwamba hana hofu na nyota wake.

“Hatuwezi kuwa na mpango mwingine tofauti na ushindi,utakuwa ni mchezo mzuri kwa timu zote,tumekuja kutafuta nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya Nusu Fainali”alisema Zahera.

Katika msafara wa kikosi hicho,Nahodha Ibrahim Ajibu hakuwapo,ambapo Kocha Zahera aliweza kueleza sababu za nyota huyo kutoambatana na timu,huku akiweka wazi kuwa hakuna kitakacho haribika.

Zahera alisema kuwa sababu za Ajibu kutokuwepo ni kutokana na kutofanya mazoezi na wenzake kwa muda mrefu kwani afya yake haikuwa vizuri.

“Mchezaji yeyote anayekosa haichangii chochote kwa Yanga kupoteza mchezo,Ajibu alianza mazoezi juzi kwahiyo hatacheza Jumamosi mechi ya Kombe la Shirikisho”alisema Zahera.