Yanga yaitakia ushindi Taifa Stars
Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema wanaitaka kila la kheri timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika mechi yao dhidi ya Uganda kesho Jumamosi.
Ten alisema Jumapili watakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya African Lyon baada ya kubadilisha ratiba ya mechi na Singida United ambayo ilikuwa ichezwe Kigoma.
"Mechi hii itakuwa ni kupiga ujangili na uuwaji wa tembo sambamba na wanaochukua meno yake tunaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi.
"Nawashukuru mashabiki wa Yanga ambao wanaendelea kuichangia timu yetu kwani pesa yao imekuwa ikisaidia mambo mengi ya kuendesha timu," alisema Ten.
"Tunapinga ujangili wa kuua na kuchukua meno ya tembo mashabiki na wapenzi wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa kupata burudani wa mechi ambayo itakuwa kali lakini dhumuni kikiwa ni hilo, " alisema Mkurugenzi wa African Lyon Rahim Zamunda.