Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga vs Waalgeria CAF damdam

Muktasari:

  • Hii itakuwa ni mechi muhimu kwa Yanga kujua itaanzaje kampeni yake kwenda kutimiza malengo ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikianza kwa kukutana na mabingwa hao wa Algeria.

YANGA itakuwa na dakika ngumu za kwanza kwenye mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, itakapokuwa mwenyeji wa MC Alger ya Algeria, itakayopigwa katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, wiki hii

Hii itakuwa ni mechi muhimu kwa Yanga kujua itaanzaje kampeni yake kwenda kutimiza malengo ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikianza kwa kukutana na mabingwa hao wa Algeria.

Iko hivi, Yanga ni kama imekuwa na nyota kukutana na timu za kutoka Algeria ambapo hata wapinzani wao hao wa msimu huu sio wageni kwani imeshawahi kukutana nao huko nyuma na kuwatibulia malengo.

Hebu tutazame namna ambavyo Yanga imekuwa ikikutananna klabu mbalimbali za Algeria ambazo zimewahi kuwakwamisha na hata kuzing’oa kibabe katika mashindano ya Afrika


USM ALGER (2022/23)

Msimu wa 2022/2023 Yanga iliweka alama kubwa ikifanikiwa kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho ambalo ilibaki kidogo tu walishushe nchini baada ya kuukosa ubingwa kwa kanuni, ikikutana na USM Alger.

Msimu huo Yanga ilicheza mechi yake ya kwanza hapa nchini, pale Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ikapoteza nyumbani kwa mabao 2-1 lakini ilipokwenda ugenini ikafanikiwa kulipa kisasi ikishinda kwa bao 1-0.

Hata hivyo matokeo ya jumla yakawa 2-2 lakini Yanga ambayo wakati huo ilikuwa ikinolewa na kocha Nasreddine Nabi ikaukosa ubingwa kwa kanuni ya kuruhusu mabao mengi nyumbani na ubingwa ukachukuliwa na Waarabu hao ambao walikutana na mechi ngumu wakiwa kwao.


CR BELOUIZDAD  (2023/24)

Msimu ulifuata Yanga ikatinga Ligi ya Mabingwa Afrika tena ambapo ikiwa chini ya kocha Miguel Gamondi kwenye makundi, ikakutana na timu nyingine kutoka Algeria CR Belouizdad, ambapo ilifungwa kisha ikalipa kisasi.

Iko hivi, mchezo wa kwanza ulipigwa Novemba 24, 2024 ikapoteza ugenini kwa mabao 3-0 lakini katika mchezo wa mwisho wa makundi ikatakiwa mabingwa hao wa Tanzania kushinda 3-0 ili kufuzu robo fainali na ukapigwa mpira mkubwa wakishinda 4-0 na kuwang’oa Waarabu.

Yanga ikiwa kwenye kundi D ikajikuta inafuzu kwenda robo fainali ikikusanya jumla ya point nane kwenye nafasi ya pili, kundi likiongozwa na Al Ahly iliyokusanya jumla ya piinti 12, wakati Belouizdad ikiwa ya tatu na pointi zao nane lakini ikiachwa kwa tpofauti mbaya ya mabao ya kufunga na kufungwa huku Medeama ya Ghana ikiwa mkiani na pointi zake nne


MC ALGER (2024/25)

Yanga ikaendelea kuwa na ziara ya Kwenda Algeria ambapo msimu wa 2024/25 ikakutana na MC Alger wakati huo mechi hizo mbili za makundi ikaongozwa na kocha mwingine Sead Ramovic rai awa Ujerumani.

Yanga ikaanza tena kwa kupoteza mchezo wa kwanza ugenini ukipigwa Desemba 7,2024 ikilala kwa kipigo cha mabao 2-0 ikionyesha kiwango cha kawaida kabisa kilichowashangaza mashabiki wengi.

Mchezo wa marudiano Yanga ikihitaji ushindi wowote ili ifuzu ikajikuta inalazimishwa sare ya 0-0, kwenye mechi ya mwisho hatua ya makundi iliyopigwa Januari 18,2025, ikikosa tiketi ya Kwenda robo fainali huku Waalgeria hao wakifuzu wakiwa ugenini.

Yanga ilimaliza ya tatu kwenye kundi lake A na pointi nane, TP Mazembe ikimaliza mkiani na pointi tano huku kinara wa kundi Al Hilal Omdurman ikiwa juu ya  msimamo na pointi 10 ikifuatiwa na MC algwer kwenye nafasi ya pili na pointi tisa.


JS KABYLIE (2025/26)

Ziara ya Yanga nchini Algeria iliendelea tena msimu uliopita, ikiwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwenye kundi lake ikakutana na JS Kabylie kutoka nchini humo ambapo safari hiyo ikafanya kweli dhidi ya Waalgeria hao lakini ikakosa kwenda robo fainali.

Iko hivi kwenye mchezo wa kwanza ugenini Yanga iliupiga mpira mwingi Novemba 28,2026 ikalazimisha sare ya 0-0 na kuonyesha matumaini kwamba inaweza kufuzu kwenye kundi hilo gumu ikikutana na timu zote zilizowahi kuchukua ubingwa wa Afrika.

Mchezo wa mwisho Yanga ilikutana na Kabylie pale Zanzibar, na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0 mechi ikipigwa Februari 15,2026 lakini hata huivyo matokeo hayo hayakuwasaidia, ikiishia makundi kutokana na kuhitaji matokeo ya timu zingine kuanguka.

Kwenye kundi lake B likaongozwa na Al Ahly na pointi  10, ikafuata AS FAR Rabat ikimaliza na pointi tisa, Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi zao nane huku Kabylie ikiwa mkiani na pointi zake tatu.


MC ALGER (2025/26)

Msimu huu Yanga itakutana tena na MC Alger na mchezo wa kwanza utakuwa wikiendi hii, ikianzia nyumbani ambapo itakutana na timu ambayo iliwanyima tiketi ya kwenda robo fainali msimu wa 2024/25. Je kipi kitabadilika kwa mabingwa hao wa Tanzania?