Yanga, Simba zaingia kimyakimya Dar
Muktasari:
- Miamba hiyo imetumia usafiri tofauti kuingia Dar wakitokea katika kambi zao za kujiandaa na mchezo huo
Dar es Salaam. Kumekucha baada ya kulikimbia jiji kwa wiki moja hatimaye Yanga na Simba zimeingia Dar es Salaam kwa njia tofauti.
Yanga ikitokea Morogoro iliingia Dar es Salaam mapema asubuhi yale wakitumia usafiri wa basi lao na kujificha hotelini wakati Simba wakitokea Zanzibar walitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3:45 asubuhi.
Simba itakuwa mgeni wa Yanga hapo kesho kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, saa 10:00 jioni.
Mashabiki wachache wa timu hiyo walijitokeza kwenye uwanja huo wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) wakijisifu kwa kusema kesho lazima wakae.