Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yaliyoimaliza Tanzanite Kombe la Dunia 2026

Muktasari:

  • Mechi tatu, vipigo vitatu, mabao mawili ya kufunga na 15 ya kufungwa ni rekodi mbaya lakini ina funzo ndani yake. Tanzanite ilianza kwa kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Brazil, ikapoteza tena kwa mabao 5-1 dhidi ya England kabla Canada kuitandika mabao 6-0.

TANZANITE Queens imeondolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia U-20 nchini Poland ikiwa na somo kubwa baada ya kukutana na uhalisia wa kiwango cha dunia.

Mechi tatu, vipigo vitatu, mabao mawili ya kufunga na 15 ya kufungwa ni rekodi mbaya lakini ina funzo ndani yake. Tanzanite ilianza kwa kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Brazil, ikapoteza tena kwa mabao 5-1 dhidi ya England kabla Canada kuitandika mabao 6-0.

Lakini ukiangalia kwa undani, Tanzanite haikutolewa na timu moja wala sababu moja. Iliangushwa na mambo kadhaa yaliyojitokeza katika mechi zote tatu. Mwanaspoti imekuchambulia mambo hayo.

DAKIKA 90 ZILIWAUA

Tanzanite ilionyesha kwamba inaweza kucheza na timu kubwa, lakini tatizo likawa ni kuendelea na kiwango hicho kwa dakika zote 90.

Dhidi ya Brazil ilifungwa 4-1, lakini hadi kipindi cha kwanza kinatamatika Tanzanite ilikuwa imesawazisha bao llilofungwa na timu hiyo lakini ilishindwa kuhimili kasi, presha ya wapinzani wake waliokuwa wanashambulia lango mara kwa mara na kipindi cha pili ikaruhusu mabao matatu.

Tatizo likajirudia dhidi ya England. Tanzania ilifungwa 5-1, huku Rachel Maltby akifunga hat-trick, ikiwamo mabao mawili ya penalty kipindi cha pili wawakilishi hao wakashindwa kutamba na kuendelea kuruhusu mabao.

Vivyo hivyo dhidi ya Canada, Tanzanite ikarudia makossa yale yale ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao moja tu, lililokuwa la kujifunga, lakini kipindi cha pili ilifunga mabao matano.

Hii ndiyo sehemu ambayo kocha Bakari Shime aliizungumza baada ya mchezo, akisema wachezaji walipoteza umakini kipindi cha pili na kuruhusu mabao kirahisi.

MAKOSA YA ULINZI

Kuruhusu mabao 15 katika mechi tatu wastani wa kuruhusu mabao matano kwa kila mechi ni  udhaifu mkubwa kwenye safu ya ulinzi ya Tanzanite.

Tanzania ilipata vipindi ambavyo iliweza kuzuia vizuri, lakini tatizo lilikuwa pale ilipofanya kosa moja ambalo lilipelekea kuwagharimu na kubadilisha kabisa mchezo.

Mfano dhidi ya Canada beki Ester Maseke alijifunga dakika ya saba wakati akijaribu kuondoa mpira uliokuwa ukielekezwa kwenye lango. Baada ya hapo Tanzania iliweza kuendelea kupambana, lakini Canada ilirudi kipindi cha pili na kufunga mabao matano.


UBORA WA WAPINZANI

Tanzania haikuwa kwenye kundi rahisi. Brazil, England na Canada zote zilikuwa na uzoefu mkubwa wa Kombe la Dunia U-20, tofauti kubwa na Tanzania ambayo ilikuwa ikishiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza.

Mfano Brazil ilikuwa tayari imeshiriki fainali hizo 12 katika historia ya mashindano hayo. Hilo pekee linaonyesha ukubwa wa uzoefu ambao ilikuwa nao kabla hata ya mpira kuanza.

England yenyewe ilikuwa inashiriki kwa mara ya nane, huku Canada ikiwa imecheza mara ya 10. Kwa maana nyingine, wakati Tanzanite ilikuwa ikiingia kwenye mashindano hayo kwa mara ya kwanza, wapinzani wake watatu walikuwa tayari wameyazoea mashindano hayo.

Na tofauti hiyo  ilionekana uwanjani. Brazil ilionyesha uwezo wa kuongeza kasi baada ya mapumziko na kuibuka na ushindi wa 4-1, licha ya Tanzania kwenda mapumziko ikiwa 1-1. England nayo ilitumia vizuri nafasi zake na kuibuka na ushindi wa 5-1, huku Canada ikifikia hatua ya kuifunga Tanzania 6-0.

UZOEFU MDOGO

Tofauti na mataifa mengine ambayo yamecheza mara kwa mara, lakini Tanzanite ilikuwa inashiriki kwa mara ya kwanza.Kwa hiyo, wachezaji walikuwa wanakutana kwa mara ya kwanza na mazingira ambayo wapinzani wao wameyazoea zaidi.

Uzoefu huo unaonekana kwenye maamuzi madogo hasa kushikilia mpira, muda gani wa kuachia, namna ya kukabiliana na presha na namna ya kurudi mchezoni baada ya kufungwa.


KUTUMIA NAFASI

Tanzania pia ilihitaji kuwa na ufanisi zaidi ilipopata nafasi.Katika mashindano makubwa kama haya, huwezi kutegemea kupata nafasi nyingi unapopata moja, lazima uitumie vizuri.

Brazil, England na Canada zilionyesha hilo. Tanzania ilipowapa nafasi, zilikuwa na uwezo wa kugeuza nafasi hizo kuwa mabao.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

MAANDALIZI

Miongoni mwa vitu ambavyo Tanzania inavyopaswa kuvichukulia siriazi ni eneo la maandalizi, kujiandaa vya kutosha kwenye mashindano makubwa kama hayo itasaidia kupunguza baadhi ya makossa madogo madogo.

Mfano kama Tanzanite ingekwenda Poland mapema na kucheza mechi za kirafiki na baadhi ya timu za ukanda huo ingesaidia kujua baadhi ya maeneo yanayovuja mapema.

Hivyo kilichoiua Tanzanite Poland siyo kwamba haikuwa na uwezo kabisa tatizo lilikuwa kwamba ilikutana na kiwango ambacho bado haijakifikia.


MSIKIE KOCHA

Kocha wa Tanzanite Queens, Bakari Shime, anasema pamoja na matokeo mabaya waliyopata kwenye mashindano hayo, safari ya Poland imewapa wachezaji nafasi muhimu ya kujifunza na kuona kwa vitendo kiwango cha soka la dunia.

Shime anasema timu yake imepata picha halisi ya ushindani wa Kombe la Dunia U-20, ikiwamo namna ya kujiandaa na kukabiliana na timu zenye ubora mkubwa. Ameongeza kuwa uzoefu huo utakuwa somo muhimu kwa Tanzania katika maandalizi ya mashindano yajayo.

“Pamoja na ugumu wa matokeo ni sehemu ya kujifunza tumeona levo ya mashindano yalivyo na namna gani ya kuyaendea.”