Watanzania kushinda zawadi Kombe la Dunia

Dar es Salaam. Katika hatua ya kuendeleza hamasa katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar, kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betway imezindua shindano maalum ambapo washindi watashinda zawadi mbalimbali za fedha taslimu.

Michuano ya Kombe la Dunia kwa sasa inazidi kupamba moto nchini Qatar ambapo timu za mataifa mbalimbali zinawania nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora.

Shindano hilo ambalo limepangwa kufanyika kwa kipindi chote cha Kombe la Dunia ambapo washindi watapata zawadi kuanzia Sh10,000, Sh1 millioni  mpaka Sh5 milioni.

Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe alisema mashabiki wa soka watakao bashiriki kupitia Airtel Money kwa dau la Sh500 watawaeza kushinda Sh10,000 ambapo jumla ya wahsindi 50 watakuwa wanazawadiwa na kuifanya kampuni hiyo kutumia Sh500,000 kwa siku.

Masaoe alisema kuwa kila wiki, watakuwa wanatoa zawadi ya Sh1 milioni kwa watakaobashiri kwa usahihi ambapo mshindi wa jumla atapatikana katika droo ya mwisho ambapo atazwadiwa Sh5 milioni.

“Lengo kubwa ni kuwazawadia mashabiki wa soka katika kipindi hiki cha shamra shamra za Kombe la Dunia na sikukuu za mwisho wa mwaka,” alisema Masaoe

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda amesema watumiaji wa huduma za Airtel Money wanaweza kupata kilicho bora zaidi katika kombe la dunia kwa kutabiri matokeo katika hatua zote za mashindano hayo.

Aliongeza kuwa shindano hilo pia ni sehemu ya ofa za msimu wa sikukuu kutoka kwa kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu kwani Airtel imedhamiria kusherehekea msimu wa sikukuu na wateja wake wapendwa.