Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapinzani wa Yanga CAF hoi

KIKOSI cha Yanga kipo kwenye mazoezi makali kikijifua kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria utakaopigwa ugenini Ijumaa ya Novemba 24, lakini wapinzani wao hao hali yao tete kwenye Ligi Kuu.

Usiku wa kuamkia jana CR Belouizdad ikicheza ugenini, ilijikuta ikipoteza mechi ya pili kwa msimu huu kwa kufumuliwa mabao 2-1 na USM Alger iliyocheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga na matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2 na kubeba ubingwa wa michuano hiyo kwa faida ya bao la ugenini.

USM Alger iliyotwaa pia taji la Caf Super Cup kwa kuifunga Al Ahly ya Misri iliyopo kundi moja na Yanga na CR Belouizdad. Kipigo cha juzi ni cha pili kwa wapinzani hao wa Yanga, kwani awali ilitandikwa nyumbani Oktoba 7 mwaka huu na timu isiyo na jina ya USM Khenchela kwa mabao 3-2 na kuifanya icheza mechi nne ikiwa na pointi sita kama za USM Alger. Belouizda imefunga mabao saba na kufungwa matano ikiwa nafasi ya 10 (kabla ya mechi za jana).

Kwenye mchezo huo, USM Alger iliipata mabao kupitia Abdoulaye Kanou dakika ya 64 na Brahim Benzaza dakika ya 90, yaliyopindua meza baada ya Belouizdad iliyotangulia kufunga bao kupitia Mcameroon Lionel Wamba dakika ya 62.

Belouizdad inashikilia ubingwa wa Algeria kwa msimu wa nne mfululizo sasa na itakuwa wenyeji wa Yanga kwenye mechi hiyo ya Kundi D itakayopigwa Novemba 24 kuanzia saa 4 usiku katika Uwanja wa Julai 5 1962 jijini Algers unaochukua watazamaji 64,200. Kabla ya kuvaana na Yanga, Belouizdad itavaana na vinara Paradou keshokutwa Jumanne kisha kumalizana na JS Kabylie Novemba 19.