Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kazi ipo kwa Majak ikiivaa Jamus kesho CECAFA

Muktasari:

  • Majak mwenye urefu wa sentimita 194 (futi 6 na inchi 4) ni miongoni mwa makipa warefu zaidi wanaoshiriki mashindano hayo hapa Kigali, Rwanda.

SIMBA inatarajiwa kukutana na mtihani mgumu kesho itakapovaana na Jamus SC ya Sudan Kusini katika mchezo wa hatua ya makundi wa Kombe la CECAFA Kagame kutokana na wapinzani wao golini kuwa na kipa mrefu balaa, Majak Mawith.

Majak mwenye urefu wa sentimita 194 (futi 6 na inchi 4) ni miongoni mwa makipa warefu zaidi wanaoshiriki mashindano hayo hapa Kigali, Rwanda.

Urefu wake umekuwa ukimwezesha kutawala eneo lake kwa kuondoa mipira ya juu kwa urahisi na kuwapa kujiamini mabeki.

Jamus tayari imeonyesha uimara wake baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-0 katika mchezo uliopita, matokeo yaliyodhihirisha uwezo wa kikosi hicho katika kutumia nguvu za mwili na kushindana kwenye mipira ya juu.

Hilo linaifanya Simba kuwa na kazi ya ziada ya kutafuta mbinu za kuvunja ukuta unaoongozwa na Majak.

Mbali na kuwa kipa wa Jamus, Majak pia ni kipa wa timu ya taifa ya Sudan Kusini. Alizaliwa katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya kabla ya kukulia Australia, ambako alianza safari yake ya soka kupitia Dandenong City, Melbourne Victory NPL, Melbourne City NPL, Port Melbourne na Dandenong Thunder, kabla ya kujiunga na Jamus mwaka 2024.

Kwa Simba, mchezo wa kesho utahitaji utulivu mbele ya lango na ubunifu mkubwa wa safu ya ushambuliaji.

Washambuliaji wake watalazimika kutafuta njia za kumpita kipa huyo mwenye kimo kirefu na uwezo mzuri wa kumiliki mipira ya juu, huku wakiepuka kutegemea krosi nyingi ambazo zinaweza kuwa faida kwa Jamus.

Baada ya kuanza mashindano kwa suluhu dhidi ya Mogadishu City, Simba inahitaji matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Hata hivyo, mbele yao kutakuwa na kipa huyo ambaye anaweza kuwa moja ya silaha kubwa za Jamus katika harakati za kuizuia Simba kupata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano hiyo.