Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wamiliki wa Man United, Arsenal na Liverpool watua New York

Muktasari:

  • Hata hivyo haikuwekwa bayana sababu za wawakilishi wa Chelsea, Manchester City na Tottenham kutohudhuria mkutano huo unaofanyika New York Marekani.

England. Vigogo wa timu tatu za Uingereza za Manchester United, Arsenal na Liverpool wamekutana kwenye mgahawa wa Swanky ikiwa ni siku chache kabla ya kupiga kura juu ya kanuni za za Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Vigogo hao Ivan Gazidis wa Arsenal, John Henry wa Liverpool, kutoka Manchester United, Joel, Avram Glazer na Ed Woodward wote kwa pamoja walijumuika kwenye chakula cha jioni jana Alhamisi.

Wajumbe kutoka klabu tatu kubwa ndio watashiriki kwenye zoezi hilo la upigaji kura wakiwakilisha klabu zingine sita kubwa England ambazo hazijapeleka wawakilishi wao.

Kanuni hiyo mpya inahusu klabu zote 20 zilizopo Ligi Kuu England ambapo kanuni inalenga mabadiliko ya  mgawanyo wa fedha kwa klabu zinazotokana na mapato ya runinga.