Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waandaaji Dar Youth League wamwagiwa sifa

DAR Pict

Muktasari:

  • Kwa upande wa U-9, Rising Youth ilitawazwa kuwa mabingwa kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aura katika mechi ya fainali. Kwenye nusu fainali za umri huo, Rising ilipata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Magnet YSA, wakati Aura ikifuzu fainali kwa kuichapa West FA kwa penalti 3-2 baada ya sare ya bila kufungana.

WAANDAAJI wa michuano ya Dar Youth League kwa vijana wenye umri chini ya miaka tisa (U-9) na kumi na moja (U-11), wamemwagiwa sifa kibao na viongozi wa timu zilizoshiriki, kutokana na uandaaji wa viwango vya juu na ufuatiliaji mzuri wa ratiba katika michuano hiyo iliyofikia tamati jana Jumapili kwenye Viwanja vya Ufundi Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mashindano hayo, Meneja wa Rising Youth, Johnson Mkonyi, aliwapongeza waandaaji hao akieleza kuwa timu yake ilipokelewa vyema na kupata huduma zote bila kukumbana na changamoto yoyote. 

Mkonyi amesema maandalizi hayo mazuri yalisaidia timu yake kuonyesha kiwango cha juu na kuibuka mabingwa wa U-9 bila kuruhusu bao, ingawa alibainisha kuwa ratiba za masomo shuleni zimekuwa zikiwapa changamoto katika kuwapata watoto kwa ajili ya mazoezi.

DA 01

Pongezi hizo ziliungwa mkono na Meneja wa Magnet Academy, Emmanuel Chanda, ambaye timu zake zilifanikiwa kutinga fainali za U-9 na U-11. 

Chanda amesifu uandaaji huo akisema kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa na kwamba uandaaji wa aina hiyo ndio unaotakiwa nchini ili kujenga msingi bora wa soka kuanzia ngazi ya chini, huku naye akitaja ratiba za shule na ibada kuwa changamoto kuu inayowakabili katika kupata muda wa kutosha wa kukaa na watoto hao.

DA 02

Katika ushindani wa uwanjani, michuano hiyo iliyoanza Jumamosi katika hatua ya makundi ilihitimishwa kwa mikwaju ya penalti kutawala mechi za hatua ya mwisho.

Kwa upande wa U-11, mechi zote za nusu fainali na fainali ziliamuliwa kwa penalti, ambapo Magnet YSA ilitwaa ubingwa baada ya kuicharaza Aura kwa penalti 5-4 kwenye fainali.

Mapema katika nusu fainali za U-11, Magnet iliiondoa Bulls kwa penalti kufuatia sare ya 2-2, wakati Aura ikiifunga West FA kwa penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya 0-0.

DA 03

Kwa upande wa U-9, Rising Youth ilitawazwa kuwa mabingwa kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aura katika mechi ya fainali. Kwenye nusu fainali za umri huo, Rising ilipata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Magnet YSA, wakati Aura ikifuzu fainali kwa kuichapa West FA kwa penalti 3-2 baada ya sare ya bila kufungana.