Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vivutio vya Tanzania vyamkosha Katibu Mkuu CAF

Muktasari:

  • Akizungumza jijini, Dar es Salaam katika hafla ya kusaini Mkataba wa Ushirikiano na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Samson amesema Tanzania ni nchi iliyopiga hatua ya kujitangaza kiutalii, jambo ambalo limeendelea kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Samson Adamu, amesema amevutiwa na vivutio vilivyopo Tanzania ambayo vitatoa nafasi kwa nchi hiyo kujitangaza zaidi katika ulimwengu wa soka duniani.

Akizungumza jijini, Dar es Salaam katika hafla ya kusaini Mkataba wa Ushirikiano na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Samson amesema Tanzania ni nchi iliyopiga hatua ya kujitangaza kiutalii, jambo ambalo limeendelea kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

"Ni furaha kubwa kwangu kuwepo leo hapa, najivunia kuona nchi iliyopiga hatua kubwa ya utalii ambayo ni moja ya sifa inayoendelea kuitangaza Tanzania nje ya mipaka ya nchi" amesema Samson.

Aidha, Samson amesema Lugha ya Kiswahili kupata nafasi ya kuidhinishwa na CAF kuwa mojawapo ya lugha rasmi ni ishara tosha ya mshikamano uliopo kati ya nchi tatu zinazoandaa AFCON 2027, ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.

"Tanzania ina historia kubwa ya kuisemea na moja ya malengo ya Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe ni kuona vivutio vilivyo nchi zote tatu vinaendelea kutangazwa duniani na kuvutia watalii mbalimbali," amesema.

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), lilifikia uamuzi wa kuidhinisha Kiswahili kiwe lugha rasmi za Shirikisho hilo, katika Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF, uliofanyika Abuja, Nigeria, Novemba 21, 2026.

Hafla hiyo ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za CAF za AFCON 2027, jijini Dar es Salaam, inayofanyika leo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na nje ya nchi.

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni Rais wa Shirikisho La Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Hussein Mohammed Rashid na Rais wa Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), Injinia Moses Magogo Hassim.