Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukame wa mabao wamtesa Kichuya

Muktasari:

Kichuya ni mmoja wa wachezaji walioisaidia Simba kutwaa ubingwa wake wa kwanza baada ya miaka mitano kupita bila ya kutwaa taji lolote, lakini msimu huu mambo yamekuwa tofauti.

Dar es Salaam. Winga wa Simba, Shiza Kichuya amesema mchezaji anayetambua kupanda na kushuka kwa kiwango chake ni rahisi kufika mbali.

Tangu msimu uanze Kichuya bado hajafanikiwa kufunga bao lolote katika michezo sita waliyocheza hadi sasa.

"Kikubwa ni kufahamu klabu inamtegemea mchezaji kufikia malengo yao, natamani kufungua akaunti yangu ya mabao kwa msimu huu kwani nauona una changamoto ya ushindani mkali.

"Nililobaini ni kuendelea kuongeza umakini wa hali ya juu kuhakikisha ninapopata nafasi nafunga, siwezi kung'ang'ania kuona ligi ngumu kwa sababu tayari wenzangu wameishafunga mabao, hivyo ni kazi kwangu kuondoa gundu hiyo," alisema Kichuya.

Msimu uliopita Kichuya alichezeshwa dakika 90, lakini kwa sasa kocha Aussems anajaribu kumpa nafasi kipindi cha pili, Ibrahim Mohamed 'Mo' ambaye alikosa namba kabisa msimu uliopita.