Uchaguzi Yanga waanza kuchezwa mahakamani
Muktasari:
Wanachama waliofungua kesi hiyo ya kikatiba namba 1/ 2019 ni Juma Magoma na Athuman Nyumba wanapinga kufanyika kwa uchanguzi huo kwa madai kuwa unakwenda kinyume na katiba ya Klabu hiyo.
Dar es Salaam. Wanachama wa Klabu ya Yanga, wamebainisha sababu za kufungua kesi ya kikatiba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kupinga kufanyika kwa uchaguzi wa kuzaja nafasi zilizoachwa ndani ya Kabla ya Yanga.
Uchaguzi huo ulipaswa kufanyika Januari 13, 2019, lakini ulishindikana kutoka na wanachama wawili kufungua kesi ya kikatiba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ijumaa iliyopita.
Wanachama hao waliofungua kesi hiyo ya kikatiba namba 1/ 2019 ni Juma A. Magoma na Athuman S. Nyumba, ambao pamoja na mambo mengine, wanapinga kufanyika kwa uchanguzi huo kwa madai kuwa unakwenda kinyume na katiba ya Klabu hiyo.
Magoma na Nyumba walifungua shauri hilo Januari 11, 2019 na kupangwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega.
Katika madai yao wakipinga kufanyika kwa uchaguzi huo kwa madai ya unakwenda kinyume na katiba ya Klabu ya Yanga ya mwaka 2010 ibara ya 7.
Ibara hiyo inaelezea utaratibu wa uanachama ndani ya Klabu ya Yanga ambao, kwanza ni kutuma maombi, ambapo maombi hayo yatapelekwa kwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, ambaye baaade yatajadiliwa na kamati tendaji.
Pia, ibara hiyo, inaelezea kuwa maombi hayo yataambatana na fomu namba YASC/U, ada ya uanachama ambayo ni Sh 12,000 pamoja ana ada ya kadi ambayo ni Sh 2000.
Pia wanadai kuwa kuna taarifa za kuwepo kwa wanachama wenye kadi feki za kieletroniki ambazo zinasaini na mhuri ambazo zinasambaa kwa baadhi ya wanachama, ambazo zinaonyesha kuwa zimetolewa na benki ya CRDB pamoja na benki ya Posta, zinazodaiwa kuwa ni kadi za uanachama wa Klabu ya Yanga, zikiwa na picha za wamiliki ambazo sio mali ya klabu hiyo.
Kwa makusudi yoyote, kadi hizo za kielektroniki zilizotolewa na CRDB na benki ya Posta, kwa namna yoyote ile haziwezi kuwa uthibitisho wa uanachama wa Yanga, kupitia kwa kuzingatia kwamba , wahusika wa hizo kadi, hawakupitia utaratibu ulioanishwa katika ibara ya 7 ya mwaka 2010 ya klabu ya Yanga.
Wanachama hao wanadai pia, kumpa mtu anachama bila kadi hiyo kusainiwa na kukong’wa muhuri wa klabu, haiwezi kutumika kuanisha uanachama wenye haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa klabu ya Yanga.
Wanadai kuwa utaratibu wa kazi za uanachama zilizotolewa na benki hizo, mpaka sasa haufahamiki wala hauna uthibitisho katika katiba ya Yanga.
Hata hivyo, ikiwa maombo hayo hayatakubaliwa watapata hasara ambayo haiwezi kufidiwa sababu kwa kuwa na matokeo ya uchaguzi ambayo hayaakisi maslahi ya wanachama na kupata viongozi ambao hawana Baraka kutoka klabu ya Yanga.
Hakimu Mtega aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, 2019, itakapotajwa.
Baadhi ya viongozi waliojiudhuru ndani ya klabu hiyo ni Yusuph Manji ambaye alikuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga, makamu wake Clement Sanga pamoja na wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
Wajumbe hao waliojiudhuru ni Hashimu Abdallah, Salum Mkemi, Omari Saidi na Ayub Nyenzi.