Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tshishimbi atoboa siri ya ubora wake Yanga

Muktasari:

Yanga ipo Visiwani Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi na leo usiku watacheza mechi ya kwanza dhiid ya Jamhuri kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Dar es Salaam. Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema siri ya ubora wake kwa sasa ni kutokana na ushindani mkubwa wa namba katika safu ya kiungo.

Tshishimbi alionyesha soka ya kiwango cha juu dhidi ya Simba ambapo alicheaza namba mbili tofauti akianza kumi na baadaye kushushwa katika nafasi aliyozoea kucheza kiungo mkabaji.

Tshishimbi alisema kikosi chao sasa kuna wachezaji wengi hasa wanaocheza nafasi ya kiungo hivyo juhudi binafsi ndio zitakazomshawishi mwalimu kuona umuhimu wa mchezaji gani kuanza kikosi cha kwanza.

"Ongezeko la Haruna Niyonzima kikosini ni changamoto kwa viungo wote tuliopo Yanga hivyo ni muda sasa wa sisi wenyewe kuendelea kupambana ili tuweze kuonyesha umuhimu wetu kikosini."

"Bado niko vizuri na nina imani na uwezo wangu sina wasiwasi na namba katika kikosi cha kwanza, lakini umuhimu wa kuonyesha ubora ni mzuri ili watu wasikusahau kama upo japo wengi wamekuwa wakiamini mimi ni mshindani kwenye mechi kubwa tu hapana inafuatana na ushindani wa wapinzani," alisema Tshishimbi.