Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tishio la virusi vya corona, Liverpool ubingwa wapewe wasipewe

Muktasari:

Ligi Kuu England kwa sasa inaisikilizia serikali kama itatangaza hali ya hatari kusiwepo mikusanyiko ya watu kutokana na maradhi hayo ya virusi vya Corona na baada ya hapo ndipo itakapochukua uamuzi itakavyohitajika.

LONDON, ENGLAND. VIGOGO wa Ligi Kuu England huenda wakalazimika kufanya mkutano wa dharura kujadili juu ya uamuzi kama Liverpool ama wapewe ubingwa wa Ligi Kuu England au wasipewe endapo ligi itashindwa kumalizika kutokana na tishio la kusambaa kwa virusi vya Corona huko Ulaya.
Kumekuwa na wasiwasi mkubwa tishio la ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Corona vikatibua matukio mengi ya michezo duniani wakati maofisa wa afya wakipambana kudhibiti kusambaa kwa maradhi hayo.
Mikusanyiko mikubwa ya watu, kama vile kwenye mechi za soka au matamasha imezuiwa kwa sababu ya hofu ya kusambaa kwa virusi hivyo tishio kwa uhai wa binadamu.
Kama itaonekana kuna hali ya hatari na ikashindikana kudhibitiwa kwa kipindi cha miezi miwili, basi jambo hilo linaweza kuifanya mikikimikiki ya Ligi Kuu England msimu huu kushindwa kumalizika.
Liverpool kwa sasa wapo kileleni kwa tofauti ya pointi 22 na walikuwa wakihitaji pointi 12 tu kabla ya mechi yao ya jana Jumamosi dhidi ya Watford ili kunyakua taji hilo ambalo litakuwa la kwanza kwao kwenye ligi tangu 1990. Zitakuwa pointi chache zaidi kama Manchester City watapoteza mechi hapo katikati.
Kwa sasa bado hakuna uamuzi kama ligi itakatishwa, hakuna kanuni za ligi zinazotoa mwongozo kitu gani kifanyike endapo msimu utashindwa kufika tamati.
Hiyo ina maana washika dau - klabu zote 20 zilizopo kwenye ligi, Bodi ya Ligi Kuu England watalazimika kuwa na mkutano wa dharura kujadili jambo hilo kupata ufumbuzi kama kufuta kabisa msimu huu au zitumike pointi zilizokusanywa hadi ilipofikia na hapo bingwa atangazwe. Jambo hilo litabaki kwenye uamuzi wa klabu kama bingwa apatikane au asipatikane mwaka huu.
Ligi Kuu England kwa sasa inaisikilizia serikali kama itatangaza hali ya hatari kusiwepo mikusanyiko ya watu kutokana na maradhi hayo ya virusi vya Corona na baada ya hapo ndipo itakapochukua uamuzi itakavyohitajika.
Utaratibu bado haupo wazi kuhusu ligi itapositishwa kutokana na janga fulani. Kwa sababu ingewezekana ligi kusitishwa zikiwa zimechezwa mechi tatu tu, pia ingeweza kusitishwa zikiwa zimebaki mechi nne tu.
Kuhusu ishu ya Liverpool kuna changamoto nyingi, kwa sababu kwa pengo la pointi walilokusanya msimu huu hadi walipofikia, itakuwa ngumu sana kuwagomea kwenye uwezekano wa kuchukua ubingwa.
Liverpool wameweka pengo la pointi 22 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili, Man City, lakini hiyo ilikuwa kabla ya mechi yao ya jana dhidi ya Watford. Lakini, kasheshe jingine litakuwa kwenye kuchukua uamuzi wa timu gani itapaswa kufuzu kucheza michuano ya Ulaya na ipo itashuka daraja.
Njia ya kawaida ya kuhesabu pointi zilizokusanywa wakati ligi inasitishwa, hiyo ina maana timu tatu zilizozo mkiani, zitashuka daraja. Lakini, shida itakuja kwa timu zenye mechi mkononi, ambao bila ya shaka wataibua madai hawatendewi haki kama ikichukuliwa uamuzi huo. Kwa sasa West Ham, Watford na Norwich City ndio timu tatu zilizopo mkiani kabla ya mechi za jana.
Wahusika wa ligi kwa sasa wala hawana shida kuhusu jambo hilo, lakini watasubiri uamuzi wa serikali kama watazuia mikusanyiko ili kuepusha kusambaa kwa janga hilo England.
Hadi kufikia sasa, zaidi ya watu 80,000 kutoka karibu nchi 50 wameambukizwa virusi vya Corona huku zaidi ya watu 2,800 wamefariki dunia.
Mashindano kama Formula One, Grands Prix Australia, Vietnam, Bahrain na China, yote yapo kwenye hatihati ya kufutwa, huku michezo ya Olimpiki ya Tokyo, Japan, iliyopangwa kufanyika kwenye kipindi cha majira ya kiangazi yajayo, yanaweza kufutwa kutokana na maradhi hayo.
Fainali za Euro 2020, ambazo zimepangwa kufanyika kwenye nchi mbalimbali za Ulaya, nazo zipo kwenye mashaka makubwa. Rais wa Fifa, Gianni Infantino alisema kuna uwezekano mkubwa wa kuzuia mechi za kimataifa za kirafiki za mwezi ujao kutokana na tishio la virusi hivyo.
Arsenal wao walimzuia mwandishi aliyekuwa amebanwa na kikohozi kuingia kwenye mkutano wao, huku staa wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min alitengezwa kwa wiki mbili baada ya kurejea England akitokea kwao Korea Kusini.
Kocha wa West Ham, David Moyes amewazuia wachezaji wake kusalimiana kwa kushikana mikono sawa na ilivyo kwa klabu ya Newcastle United.
Mabosi wa Ligi Kuu England bado hawajafanya uamuzi wa kusitisha suala la wachezaji kushikana mikono kabla ya mechi kuanza.