Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tatoo za Chama zina ujumbe maalum, si mapambo tu

Muktasari:

  • Chama ambaye ni mmoja wa wachezaji gumzo hapa Kigali, Rwanda kwenye michuano ya Kagame, alisema tatoo hizo ambazo zipo kwenye mkono wake wa kushoto si kwa ajili ya mapambo pekee, bali ni kumbukumbu ya watu muhimu katika maisha yake ambao wamekuwa sehemu kubwa ya safari yake ya soka.

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama, amefichua sababu ya kuchora tatoo mbalimbali kwenye mwili wake, akisema kila alama aliyonayo ina ujumbe maalum unaohusiana na familia yake.

Chama ambaye ni mmoja wa wachezaji gumzo hapa Kigali, Rwanda kwenye michuano ya Kagame, alisema tatoo hizo ambazo zipo kwenye mkono wake wa kushoto si kwa ajili ya mapambo pekee, bali ni kumbukumbu ya watu muhimu katika maisha yake ambao wamekuwa sehemu kubwa ya safari yake ya soka.

Kiungo huyo wa Zambia alisema majina yaliyochorwa kwenye mwili wake yanawakilisha mke wake, watoto wake na watu wa familia yake ambao wamekuwa wakimpa nguvu katika maisha na kazi yake.

“Haya ni majina ya familia yangu, kila alama ninayo kwenye mwili wangu ina jina maalum. Kuna jina la mke wangu na watoto wangu,” alisema Chama. “Mimi ni mtu ninayeamini sana katika familia. Ninaithamini familia yangu kwa sababu ndiyo mashabiki wangu wakubwa. Wananipa motisha na kunifanya niendelee kupambana,” aliongeza.

Chama alisema licha ya changamoto mbalimbali anazokutana nazo katika soka, familia yake imekuwa nguzo muhimu inayomsaidia kubaki imara na kuendelea kutafuta mafanikio. Kiungo huyo amekuwa akionekana mara kwa mara akishirikisha maisha yake ya kifamilia kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo linaonyesha ukaribu wake na watu wake wa karibu.

Kuhusu mke wake ambaye mara nyingi huonekana akimuunga mkono kwenye mechi mbalimbali na hata kujifunza mambo ya soka kutoka kwake, Chama alimuelezea kwa kifupi.

“Ni mtu wa ajabu sana, ni mtu ambaye amekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu na safari yangu ya soka,” alisema.

Chama na mastaa wengine wa Simba walishuka dimbani jana, Jumanne kucheza mchezo wa pili dhudi ya Jamus katika michuano ya Kagame ambayo wanaitumia kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.