Tarehe ya Uchaguzi Mkuu Simba hadharani, matawi yajulishwa
Muktasari:
- Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu kwenda kwa matawi ya klabu hiyo, uchaguzi huo utakuwa ni miongoni mwa agenda za mkutano mkuu wa Simba.
Uongozi wa klabu ya Simba umepanga Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo kufanya Januari 30, 2027 katika eneo ambalo bado halijatangazwa.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu kwenda kwa matawi ya klabu hiyo, uchaguzi huo utakuwa ni miongoni mwa agenda za mkutano mkuu wa Simba.
“Kwa mujibu wa katiba ya Simba Sports Club, Ibara 21(1) ya Katiba ya Simba Sports Club, 2018 (iliyofanyiwa marekebisho November, 2025) na kusajiliwa 18.02.2026, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Simba Sports Club wanataarifiwa kuwa Mkutano Mkuu wa kawaida utafanyika Siku ya Jumamosi 30.01.2027 kuanzia saa 3 asubuhi.
“Taarifa ya mahali utakapofanyika mkutano huo na ajenda mahususi itawajia baadae, kwa mujibu wa Ibara 21(2) ya Katiba ya Simba Sports Club.
“Tunataraji kuwa Mkutano huo utaambatana na agenda ya uchaguzi kwa mujibu ibara ya 20(6) na 22(i) ambapo utasimamiwa na kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ambapo taratibu zote zitaelekezwa kutoka kwa mamlaka husika,” imesema barua hiyo.
Kupangwa kwa tarehe hiyo kunaenda kinyume na maelekezo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Wakili Kiomoni Kibamba kwamba Uchaguzi huo ufanyike kabla ya muda wa uongozi wa sasa kukamilika Januari 29, 2027.
“Iwe mvua iwe jua, uchaguzi lazima ufanyike. Kwa kuwa uchaguzi ulifanyika Januari 29, 2027, maana yake ukomk wa uongozi wao ni Januari 29, 2027,” alinukuliwa Kibamba.