Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika JKT Queens amtaja Opah Clement

BAHATI Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo alianza kujulikana  katika mashindano ya vijana baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano ya CECAFA chini ya miaka 17 akiweka kambani mabao 10.

MSHAMBULIAJI wa JKT Queens, Bahati Steven amesema Opah Clement ni miongoni mwa wachezaji aliokuwa akiwafuatilia tangu anaanza maisha ya mpira na kutamani siku moja kufika alipo nahodha huyo wa Twiga Stars.

Bahati aliyesajiliwa na JKT Queens msimu huu akitokea Bunda Queens ya Mara, amekuwa miongoni mwa wachezaji vijana wanaotazamwa kuwa na ubora  katika Ligi Kuu ya Wanawake kutokana na uwezo aliouonyesha.

Bahati amesema kumfuatilia Opah kulimpa hamasa ya kuendelea kupambana katika soka, kutokana na nidhamu ya upambanaji anayoonyesha mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga Al Ula ya Ligi Kuu ya Wanawake Saudia.

“Wapo wengi nawafuatilia na najifunza vitu kwao, lakini Opah kwa sababu ana nidhamu ya kazi, pia ni fundi wa kufumania nyavu, vimenifanya nimkubali zaidi,” amesema Bahati

Kwa mujibu wa Bahati, moja ya mambo yanayompa furaha ni ndoto yake ya kucheza pamoja na mchezaji aliyekuwa akimtazama sasa imetimia baada ya kukutana naye katika kikosi cha timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars.

Mshambuliaji huyo alianza kujulikana  katika mashindano ya vijana baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano ya CECAFA chini ya miaka 17 akiweka kambani mabao 10.

Kabla ya hapo alilelewa na kukuzwa kwenye kituo cha Bunda Queens ambacho kimetoa nyota wengi wanaokiwasha Ligi Kuu ya Wanawake.