Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida Black Stars yasaka ubani jijini Arusha

SINGIDA Pict

Muktasari:

  • Singida inaingia katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Nyayo, huku ikisaka rekodi ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa mara ya pili kihistoria, baada ya kufanya hivyo, msimu wa 2025-2026.

KIKOSI cha Singida Black Stars kimeendelea na maandalizi yake jijini, Arusha kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika, dhidi ya Tusker FC ya Kenya, itakayopigwa, Oktoba 18, 2026.

Singida inaingia katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Nyayo, huku ikisaka rekodi ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa mara ya pili kihistoria, baada ya kufanya hivyo, msimu wa 2025-2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Singida, Hussein Massanza, amesema baada ya mechi ya juzi ya timu hiyo ya Ligi Kuu Bara waliyochapwa bao 1-0, dhidi ya Coastal Union, kikosi hicho kinajiandaa kuikabili Tusker FC.

SINGI 01

“Baada ya mechi yetu ya Ligi Kuu na Coastal Union kumalizika tumeanza maandalizi ya haraka kwa ajili ya kuikabili Tusker FC, tumeweka kambi ya muda jijini, Arusha kwa sababu hali ya hewa ni sawa na ya Kenya tutakayochezea,” amesema Massanza.

Massanza amesema benchi la ufundi la kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu, Mkongomani Papy Kimoto halijaridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo, jambo ambalo anaendelea kulifanyia kazi kabla ya kucheza ugenini dhidi ya Tusker.