Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaidhalilisha Mashujaa, ikiipiga sita

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuwa wababe kwenye ligi ikifisha pointi 24 baada ya mechi zake nane, ikizidi kujitanua juu ya msimamo wa ligi.

Simba imeendeleza moto wake ikifanikiwa kuichapa kwa kipigo kikali cha mabao 6-1  Mashujaa FC huku wekundu hao wa Msimbazi wakiendelea kujikita juu ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ilifanikiwa kumaliza kipindi cha kwanza kwa ikiongoza kwa mabao 2-0 yakifungwa na Libasse Gueye kwa bao la shuti la mbali katika dakika ya 16 kisha Ellie Mpanzu ambaye amefunga mabao mawili kwenye mchezo huo akifunga la pili katima dakika ya 32 na kuwafanya wenyeji waende mapumziko wakiwa na uongozi wa mabao mawili.

Dakika tatu kabla ya mapumziko Mashujaa ilipata pigo baada ya winga wake Hassan Kabunda kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kunaswa na FVS akimpiga kiwiko beki Antony Mligo.

SIMB 01

Awali mwamuzi Abdi Wajihi kutoka Tanga alimpa winga huyo kadi ya njano ambapo baada ya kujiridhisha kupitia marudio ya video alibaini Kabunda kutumia kiwiko na kubadilisha maamuzi yake.

Kipindi cha pili Simba ilirejea kwa nguvu na kufanikiwa kutengeneza mabao mengine manne ambapo Anicet Oura akaandika bao la tatu katika dakika ya 53 kisha Mpanzu akaweka bao lake la pili na la nne kwa timu yake katika dakika ya 58.

Morris Abraham ambaye aliingia kipindi cha pili akaweka wavuni bao la tano katika dakika ya 61 kisha beki Ismael Toure kumalizia msumari wa sita katika dakika ya 68.

SIMB 02

Mshambuliaji wa Mashujaa Seleman Bwenzi akiingia kutokea benchi akamuharibia hati safi kipa wa Simba Tanji Kassali kwa kuifungia timu yake bao kali katika dakika ya 63 kwa shuti kali lililomshinda kipa huyo likigonga mwamba na kujaa wavuni.

SIMB 03

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuwa wababe kwenye ligi ikifisha pointi 24 baada ya mechi zake nane, ikizidi kujitanua juu ya msimamo wa ligi.