Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yafikia rekodi ya Arsenal, Chelsea  

Muktasari:

  • Simba imeuanza msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa ushindi katika mechi zote tatu, lakini kila mchezo imeumaliza ikiwa na mchezaji pungufu.

Klabu ya Simba, imeingia katika orodha adimu ya timu kubwa zilizowahi kupata kadi nyekundu katika mechi tatu mfululizo, baada ya mchezaji wake wa tatu kutolewa katika mchezo dhidi ya Singida Black Stars, uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Airtel, Singida.

Simba imeuanza msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa ushindi katika mechi zote tatu, lakini kila mchezo imeumaliza ikiwa na mchezaji pungufu.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar, beki wa kulia, David Kameta 'Duchu' alitolewa kwa kadi nyekundi, dhidi ya Pamba Jiji, kiungo Ibraheem Jabaar alionyeshwa kadi nyekundu huku beki wa kushoto, Anthony Mligo akiwa mchezaji wa tatu kutolewa kwa adhabu dhidi ya Singida Black Stars.

Arsenal iliwahi kukutana na changamoto kama hiyo msimu wa 2011/12 wa Ligi Kuu England.

Kama ilivyotokea kwa Simba,Arsenal ilipata kadi nyekundu katika kila moja ya mechi zake tatu za kwanza.

Winga raia wa Ivory Coast,Gervais Yao Kouassi. 'Gervinho' alitolewa kwa kadi nyekundi katika sare ya 0-0 dhidi ya Newcastle United, mchezo ulipigwa Agosti 13, 2011, Emmanuel Frimpong akaonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Liverpool,mchezo ulipigwa Agosti 20,2011.

Mwingine ni Carl Jenkinson ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu katika kipigo cha mabao 8-2 ilichokipata Arsenal dhidi ya Manchester United,mchezo ukipigwa Agosti 28, 2011.

Iliripotiwa kuwa, Arsenal ndiyo ilikumbana na kadi tatu nyekundu kwa muda mfupi zaidi katika historia ya Ligi Kuu England wakati huo, ikiwa imepata moja katika kila mechi zake tatu za kwanza.

Tofauti ni kwamba, Arsenal ilianza vibaya msimu huo, ikipata pointi moja pekee katika mechi tatu za mwanzo, wakati Simba imefanya hivyo ikiwa na asilimia 100 ya ushindi.

Chelsea ni klabu nyingine kubwa na maarufu iliyowahi kukutana na majanga hayo msimu wa 2025/26.

Robert Sánchez alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Manchester United, uliopigwa Septemba 20, 2025, Trevoh Chalobah akafuata dhidi ya Brighton, mchezo ukipigwa Septemba 27, kabla ya João Pedro kutolewa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, uliopigwa Septemba 30, 2025.

Kwa hiyo Chelsea ilikuwa na kadi nyekundu katika mechi tatu mfululizo, ingawa kuna tofauti moja muhimu, mechi ya tatu ilikuwa ya Ligi ya Mabingwa.

Chelsea baadaye iliendelea kuwa na tatizo kubwa la nidhamu, ikimaliza msimu wa 2025/26 ikiwa na jumla ya kadi nyekundu 10 katika mashindano yote.

Mfululizo wa kadi nyekundu pia umewahi kuonekana kwa timu nyingine katika ligi kubwa za Ulaya.

Kilichostua kwa Simba ni kwamba imefanya hivyo katika mechi tatu za kwanza kabisa za msimu, ikiwa na wachezaji watatu tofauti,lakini imefanikiwa kushinda zote tatu.

Simba ilizindua kampeni zake za msimu huu kwa kuikabili Kagera Sugar na kushinda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera, kisha ikashinda mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kabla ya juzi Jumamosi kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars kwenye Uwanja wa Airtel, Singida.

Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'akizungumzia matukio hayo ya kadi nyekundi kwa timu yake hiyo alisema: "Chamsingi wachezaji wawe makini kwasababu kuna teknolojia(FVS) inatumika, kama hawatakuwa makini kadi nyekundu zitashuhudiwa kila siku.Kama adhabu zinatolewa kwa kuzingatia kilichotokea hatuwezi kulaumu,".

Wakati huo huo, mahasimu wa Simba, Yanga watashuka dimbani leo kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo,Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Yanga itaingia uwanjani ikitaka kuendelea rekodi ya ushindi wa asilimia mia moja tangu kuanza kwa msimu huu, wakati JKT Tanzania itahitaji kusaka ushindi wa kwanza msimu huu.

Timu hizo kila moja itacheza mchezo wa tatu, Yanga ilianza msimu kwa kuumana na Namungo na kushinda mabao 3-1, kisha ikaichakaza Coastal Union mabao 4-1.

JKT kwa upande wake, ilizindua kampeni kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya TRA United, kisha ikatandikwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania.