Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaficha silaha zake Milford Lodge Zambia

Muktasari:

. Nyota wa Simba wajichimbia hoteli ya maana hapa Nkana Street road 251 Kitwe Zambia.

Kikosi cha Simba kimefikia katika hoteli ya The Milford Lodge iliyopo hapa Kitwe Zambia tangu jana Alhamisi.

Hoteli hiyo ambayo kwa siku unalipia Dola 100 kwa chumba kimoja ipo mahala kwenye utulivu na ukimya wa hali ya juu.

Mapema leo Mwanaspoti ilishuhudia nyota wa Simba wakipata chai katika ukumbi uliokuwa ndani ya hoteli hiyo.

Wachezaji wa Simba muda mwingi wamekuwa nadra kuonekana wakikatiza katika hoteli hii.

Muda mwingi wachezaji wote walionekana kujifungia vyumbani mwao huku umakini na utulivu ukiwa mkubwa ndani ya hoteli hii.