Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shida ya KVZ ipo hapa

KVZ Pict

Muktasari:

  • KVZ ambayo ni bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, tayari imecheza mechi mbili za Ligi Kuu Zanzibar na jana Jumapili ilishuka dimbani kukabiliana na Raskazone.

KATI ya mechi nane ambazo KVZ imecheza msimu huu za mashindano tofauti, imeonekana kutokuwa kwenye kiwango kizuri, huku shida ya matokeo hayo ikibainika kwenye maeneo mawili ambayo ni ulinzi na ushambuliaji.

KVZ ambayo ni bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, tayari imecheza mechi mbili za Ligi Kuu Zanzibar na jana Jumapili ilishuka dimbani kukabiliana na Raskazone.

Timu hiyo kabla ya jana, ilikuwa imecheza jumla ya mechi nane za mashindano tofauti, ikishindwa kupata ushindi katika dakika 90, huku ikiruhusu mabao 16 na kufunga matatu pekee.

Jambo la kushangaza ni timu hiyo ina washambuliaji sita ambao ni Mohamed Massoud Dola, Abdalla Iddi ‘Pina’, Nature Mwakilembe, Akram Muhina ‘Haaland’, Mohammed Hussein ‘Banega’ na Mudrik Abdi Shehe ‘Gonda’, lakini wameshindwa kufunga mabao ya kutosha licha ya kuonekana nafasi nyingi zinatengenezwa. Mabao yao matatu yaliyofungwa, mawili yametoka kwa washambuliaji ambao ni Haaland na GOnda, lingine alifunga kiungo, Yakoub Moh’d.

KV 01

Kocha Mkuu wa KVZ, Hababuu Ali amesema washambuliaji wa timu hiyo bado hawatumii nafasi vizuri kwa sababu wanatengeneza nafasi za kutosha lakini shida imekuwa kwao kumalizia.

“Straika bado hawatumii nafasi kwa sababu tunatengeneza nafasi za kutosha, mechi dhidi ya JKU ilikuwa ngumu, lakini kila aliyekuwepo uwanjani aliona kama tulicheza vizuri kuliko wapinzani wetu japo shida inakuja palepalek kuzitumia nafasi,” amesema Hababuu.

KV 01

Kocha huyo amebainisha mechi dhidi ya Polisi ndiyo ilikuwa tatizo upande wao kwani wachezaji hawakujituma, huku akisema bado timu haijapata muunganiko mzuri kwa kuwa wachezaji wengi ni wapya.

Akizungumzia mechi za kimataifa, kocha huyo amesema hilo halina mjadala kwa sababu ya uchanga walionao kwenye mashindano makubwa.

Ikumbukwe kabla ya Ligi Kuu Zanzibar, KVZ ilianza kushiriki michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika Rwanda ikicheza mechi tatu na kuruhusu mabao manane, ikiondoka bila ya kufunga bao wala pointi.

KV 03

Ikarejea Zanzibar kucheza Ngao ya Jamii dhidi ya JKU, dakika tisini zilimalizika kwa sare ya 2-2, ikashinda kwa penalti 8-7.

Baada ya hapo, ikacheza mechi mbili za Ligi Kuu Zanzibar ikianza kwa kufungwa bao 1-0 na Polisi, kisha sare ya 1-1 na JKU.

KV 01

KVZ katika uwakilishi wake wa Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, KVZ ilipoteza mechi zote mbili na kutupa nje hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao 4-0.

Kwa jumla, matokeo ya KVZ mechi nane ilizocheza msimu huu katika mashindano tofauti yapo hivi; Rayon Sports 2-0 KVZ, Al Hilal 4-0 KVZ, Tusker 2-0 KVZ, KMKM 2-2 KVZ, Polisi 1-0 KVZ, Asswehly 1-0, KVZ 0-3 Asswehly na JKU 1-1 KVZ.