Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SBL yaipongeza Stars

Dar es Salaam. Wadhamini wakuu wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)  wamepongeza ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger na kuweka matumaini ya kufuzu fainali za Afcon zilizopangwa kufanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Taifa Stars ambayo ipo kundi F, kwa sasa imeshika nafasi ya pili kwa kukusanya jumla ya pointi saba (7) zilizotokana na michezo mitano huku ikihtaji pointi moja tu ili kuungana na Algeria kufuzu hatua ya fainali.

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa mwisho Septemba 4 dhidi ya Algeria mjini Algiers.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi amesema kuwa wana uhakika kuwa taifa Stars itafuzu na kuendelea kuitangaza nchi kupitia mashindano ya Afcon.

Alisema kuwa ushindi huo ni faraja kwa SBL ambayo iliamua kuwekeza katika timu hiyo kwa lengo la kuleta tija katika maendeleo ya soka nchini.

“Tumewekeza mamilioni ya fedha kwa kuidhamini Taifa Stars ambapo lengo letu kubwa ni kuchangia maendeleo ya soka nchini. Furaja yetu ni kuona timu inafanya vizuri na sasa ipo katika nafasi kubwa ya kufuzu. Tunaamini watafuzu na kuipeperusha vyema bendera ya nchi katika mashindano hayo makuba ya Afrika,” alisema Anyalebechi.

Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa timu ya Taifa, waliamua kuwekeza kwa Sh 5.1 billioni kuanzia mwaka 2017 na sasa matunda ya uwekezaji huu yanaonekana.

Mbali ya kuwekeza Taifa Stars, SBL pia inadhamini lifi kuu ya Wanawake Tanzania, Serengeti Lite Premier League.

 Kwa upande wake, kocha mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche alisema kuwa nguvu yako kubwa kwa sasa wanailekeza kwenye mechi dhidi ya Algeria ambayo ndiyo itaamua hatma yao.

“Wachezaji wamefanya vyema sana na wanastahili pongezi kubwa pamoja na wadhamini, SBL,” alisema Amrouche.